METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, July 16, 2018

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko afanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa Njombe

Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Mashaka Biteko (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Christopher Ole Sendeka (kulia) baada ya kufanya mazungumzo mafupi, jana asubuhi Julai 16, 2018.

Mhe.Biteko alifika ofisini kwa Mhe.Ole-Sendeka akiwa njiani kuelekea mkoani Ruvuma kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katika mazungumzo hayo Mhe. Ole-Sendeka alimweleza Mhe.Biteko kuhusu utafiti wa madini ya chuma aina ya Liganga na Mchuchuma ambayo yanapatikana mkoani Njombe na kwamba taratibu za kisheria zinaendelea kufanyika kabla ya mwekezaji kusaini mkataba wa kuanza uchimbaji wa madini hayo. 

Mhe.Biteko alisema serikali imeweka taratibu za kuhakikisha mikataba yote ya uchimbaji madini inayosainiwa nchini inakuwa na maslahi baina ya pande zote (wananchi, serikali pamoja na mwekezaji).
Picha na George Binagi, Njombe
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com