METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, July 20, 2018

WATU ELFU TISINI KUPIMWA VVU MKOA WA IRINGA

 Mkuu wa mkoa Iringa Amina Masenza akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha upimaji wa VVu
Baadhi ya wadau na viongozi wa mkoa wa Iringa waliohudhuria kwenye tukio la uzinduzi wa kuhamasisha upimaji VVU mkoa wa Iringa.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

SERIKALI ya mkoa wa Iringa inatarajiwa kuwapima VVUtakribani wananchi elfu tisini (90,000) kwa lengo la kudhibiti ongezeko la ugonjwa wa ukimwi na kuwaanzishia kutumia ARV KWA wale AMBAO wamekututwa  na VVU.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, kwa kusema kuwa kuwa wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti UKIMWI kwa kushirikiana na TACAIDS na wadau wa USAID tulonge afya na kuzinduliwa siku ya tarehe 24 julai 2018 katika viwanja vya Mwembetogwa.

kamapeni hii itahamasisha mkakati mpya wa serikali wa upimaji wa VVU na kuanza matumizi ya ARV mapema kwa wale ambao watakuwa wamekugulika kuwa na maambukizi ya VVU,kupitia kampeni ya “Furahayangu, pima ujitambue,ishi” ujumbe huo mutakufanya mtu uliyepima kuwa huru. Alisema Masenza.

Masenza alisema kuwa serikali ya awamu ya imedhamilia kuhakikisha kuwa inapambana kuhakikisha inapunguza maambukizi ya ukimwi na kufikia lengo la “TISINI TATU” ifikapo mwaka 2020 na wananchi asilimia tisini wawe wamejua hali zao za maambukizi na wawe wamepimwa VVU ILI waweze kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU.

Aidha Masenza alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa umejipanga kuhakikisha vitendanishi na dawa ARV zipo za kutosha katika kila kituo kinatoa huduma ili kuweza kuwahudumia vizuri na kuwaanzishia dawa watakagundulika kuwa na maambukizi ya VVU na Ukimwi.

Masenza alisema kuwa serikali ya mkoa  imevitaka vyombo vya habari mkoani hapo kushiriki kuhamasisha jamii
Hivyo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki maandamano yatakayoanzia bustani ya Manispaa kisha uwanja wa Mwembetogwa.
Alisema kuwa mwandishi bora atapewa zawadi kulingana na vigezo vitakavyo wekwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com