Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati
wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania
linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Baadhi ya wananchi pichani wakimsikiliza Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisikiliza maelezo ya utunzaji fedha mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha Tanzania wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018.
Na Mathias Canal-WK, Mwanza
Serikali imetangaza Kiama kwa
viongozi na baadhi ya watendaji wa vyama vya ushirika waofanya ubadhilifu wa
Mali za ushirika kwa manufaa yao pekee pasina kuwanufaisha wanachama wote.
Imeelezwa kuwa ubadhilifu wa
rasilimali za ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama
vya ushirika umekuwa ni tatizo sugu na hata kuwakatisha tamaa baadhi ya
wananchi kujiunga na vyama hivyo.
Kalipio kwa wabadhilifu hao
limetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Leo 6 Julai 2018 wakati
wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania
linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
Kongamano hilo la Siku mbili
litaambatana na maonesho ya bidhaa na shughuli zinazofanywa na vyama hivyo vya
ushirika kote nchini ambapo wanachama watapata fursa ya kubadilishana uzoefu,
na kujadili mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa
sekta ya ushirika nchini.
Dkt Tizeba aliwasisitiza
washiriki wa kongamano hilo kutumia vizuri siku hizo mbili za kongamano hilo
kwa ajili ya ustawi wa Maendeleo ya vyama vya ushirika na kujadili kwa kina
namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa vyama hivyo.
Alisema kuwa kauli mbiu ya siku
ya ushirika Duniani kwa mwaka 2018 isemayo "Ushirika kwa ulaji na
uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma" inakumbusha kwamba vyama vya
ushirika sharti vihakikishe vinajitangaza na kutafuta Masoko ya bidhaa na
huduma zake kwa jamii nzima.
Mhe Waziri wa Kilimo Dkt Charles
Tizeba aliongeza kuwa serikali inatambua kuwa ushirika ni nyenzo muhimu ya
kuwasaidia wananchi katika upatikanaji wa mtaji na kuwawezesha kuunganisha
nguvu zao za kiuchumi katika kujiendeleza kiuchumi.
Alisema kuwa zipo juhudi kubwa
zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha
wananchi wengi zaidi wanahamasishwa na hatimae kujiunga kwenye vyama vya
ushirika kulingana na shughuli zao za kiuchumi ili kuondoa dhana kuwa vyama vya
ushirika ni kwa ajili ya Kilimo cha Mazao ya biashara ya nchi za nje.
Sambamba na hayo Mhe Tizeba
ameitaka Tume ya Maendeleo ya ushirika na shirikisho la vyama vya ushirika
kuendelea kuwahamasisha wananchi kuendelea kutambua umuhimu wa kujiunga katika
vyama vya ushirika kulingana na shughuli za wananchi mfano ushirika wa Viwanda,
Madini, Ufugaji, Usafirishaji, Uvuvi na Kilimo.
Aliongeza kuwa serikali
inatambua na kuthamini mchango wa ushirika wa Taifa katika kuyafikia malengo ya
milenia na malengo mbalimbali ya nchi kama uimarishwaji wa sekta ya viwanda,
Kilimo, uvuvi na biashara na kuchangia katika ongezeko la kipato kwa wananchi
na hatimaye kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment