METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 5, 2018

WAZIRI WA KILIMO AAGIZA KUKAMATWA WAFANYABIASHARA WANAOINGIZA SUKARI NA MCHELE KWA MAGENDO NCHINI

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Leo 5 Julai 2018 ameliagiza jeshi la Polisi kuwakamata wafanyabiashara wanaouza sukari na mchele kinyume cha sheria, Kanuni na taratibu za nchi.

Maagizo hayo yametolewa baada ya Mh. Waziri wa Kilimo akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Miraji Kipande kufanya ziara ya kushtukiza kwenye maduka makubwa ya Shoppers Super Market Ltd Jijini Dar es salaam.

Katika ziara hiyo ya kushtukiza  Mh. Waziri alikuta Sukari na mchele iliyokuwa ikiuzwa na wafanyabiashara hao kinyume na taratibu za nchi. Sukari iliyokutwa ilikuwa  imefungashwa katika ujazo wa kilo moja moja na zilisomeka kuwa zimetoka nchini Mauritius na Uingereza ambazo ziliingizwa nchini bila ya kuwa na kibali cha Waziri Mkuu au Bodi ya Sukari Tanzania ambayo ipo chini ya Wizara ya Kilimo.

Kwa sasa wafanyabiashara hao wametiwa nguvuni na suala hilo lipo polisi kwa ajili ya uchunguzi na taratibu zingine za kisheria pindi uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa hao watapandishwa kizimbani.

MWISHO.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com