METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, July 22, 2018

MBUNGE WA ILEMELA AWATAHADHARISHA WANANCHI KUFUATA SHERIA ZA ARDHI

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amewatahadharisha wananchi wa jimbo lake kufuata sheria za ardhi na kuacha kununua maeneo kutoka kwa wenyeviti wa serikali za mitaa.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa mtaa wa Mhonze kata ya Shibula ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kawaida ya kuzungumza na wananchi wa jimbo lake, kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo, kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero na changamoto zinazowasilishwa kwake na wananchi hao  akishirikiana na wataalamu wa manispaa ya Ilemela ambapo amewaasa kuacha kununua maeneo kienyeji kupitia kwa wenyeviti wa mitaa kwani hawana mamlaka ya kufanya hvyo kisheria kitendo kinachosababisha kuongezeka kwa migogoro ya ardhi

‘… Maeneo mengi watu wamejenga bila kufata utaratibu pamoja na kwamba tumeshatoka kwenye vijijini tupo kwenye mitaa kwa maana ya manispaa, na unapokuwa manispaa mwenyekiti wa mtaa hana mamlaka yeyote na ardhi,  ardhi inakuwa chini ya sheria namba 8 ya mwaka 2007 ya mipango miji, eneo lote linapangwa, kwa hyo mwenyekiti wa mtaa hana sauti, hawezi kuuza ardhi wala hawezi kufanya chochote …’ Alisema

Aidha Dkt Mabula amemshukuru Rais Mhe Dkt John Magufuli na wasaidizi wake kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali inayonufaisha wananchi wake ikiwemo bilioni 1.5 kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ndani ya jimbo lake,   milioni 500 kwaajili ya kituo cha afya Karume, milioni 400 kituo cha afya Buzuruga, 400 kwaajili ya kituo cha afya  Ilemela, milioni 700 kwaajili ya kituo cha afya Kirumba na milioni 155 kwa zahanati zote zzilizopo ndani ya jimbo lake huku milioni 366 zikitolewa mpaka sasa kama mikopo kwaajili ya kuviwezesha vikundi vya kina mama, vijana na walemavu kutekeleza shughuli mbalimbali za kujikwamua kiuchumi

Kwa upande wake Diwani wa kata aya Shibula Mhe Swila Dede amempongeza mbunge huyo kwa juhudi zake za kumleta Waziri wa nishati jimboni humo huku akimuomba kumsaidia vijiji vya Semba ‘A’, Semba ‘B’ na Bugala  viweze kunufaika na mpango huo wa umeme vijijini REA.

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'

Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
22.07.2018.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com