Waziri wa Madini Angellah Kairuki,
akifuatilia jambo wakati Kaimu
Mkurugenzi Takwimu za Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa akiwasilisha mada
Mchango wa Shughuli za Madini katila Pato la Taifa.Kushoto ni Naibu Waziri wa
Madini, Doto Biteko.
Kaimu
Mkurugenzi Takwimu za Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa akiwasilisha mada
ya Mchango wa Shughuli za Madini katila Pato la Taifa kwaWaziri wa Madini,
Angellah Kairuki (hayupo pichani) na Menejimenti ya Wizara pamoja na watumishi kutoka Taasisi zake wanaofuatilia.
Kaimu
Mkurugenzi Takwimu za Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa akiwasilisha mada
ya Mchango wa Shughuli za Madini katila Pato la Taifa kwaWaziri wa Madini,
Angellah Kairuki (hayupo pichani) na Menejimenti ya Wizara pamoja na watumishi kutoka Taasisi zake wanaofuatilia.
Na Asteria Muhozya, Dodoma
Waziri wa Madini Angellah Kairuki ameitaka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) kuisaidia wizara iweze kubaini maeneo maalum ya kuzingatia
yatakayowezesha kuongeza mchango wa Sekta katika Pato la Taifa.
Aliongeza kuwa, ushauri
utakaotolewa na NBS utaisaidia wizara kujipanga zaidi kuhusu namna ya kutumia
fursa zilizopo katika sekta husika na sekta nyingine ili kuhakikisha kuwa pato
la Sekta linaongezeka.
Waziri Kairuki aliyasema hayo tarehe 23 Julai, Makao Makuu ya
Wizara jijini Dodoma, wakati wa kikao kati ya Menejimenti ya Wizara na Taasisi
zake ambapo Kaimu Mkurugenzi Takwimu za Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa,
aliwasilisha mada kuhusu Mchango wa Shughuli za Madini katila Pato la Taifa.
Kikao hicho kinafuatia maelekezo ya Waziri Kairuki aliyoyatoa
kuhusu wizara kukutana na NBS ili isaidie kuona ni namna gani wizara itaongeza
mchango wake katika pato la taifa kutoka asilimia 4.8 ya sasa kufikia asilimia
10 ifikapo mwaka 2025.
Pia, Waziri Kairuki aliwataka Watendaji wa wizara na taasisi
husuan Tume ya Madini kupitia kila vifungu vya Sheria ya Madini na kuhakikisha
kuwa vinatekelezwa kikamilifu.
Aidha, Waziri Kairuki alimshukuru mtaalam huyo na kuikaribisha
ofisi ya NBS kuendelea kuishauri wizara kuhusu masuala ya takwimu kwa lengo la
kuipeleka mbele sekta ya madini.
Wakati akiwasilisha mada, Musolwa aliishauri wizara kusimamia
vizuri mianya ya mapato yatokanayo na madini pamoja na kuongeza juhudi
katika kuhakikisha inapata taarifa za kutosha hususan katika madini ya ujenzi.
Pia, aliishauri wizara kuhusu kufanya tafiti za madini katika
maeneo mbalimbali ya nchi jambo ambalo litaiwezesha kupata taarifa
zitakazosaidia katika ukusanyaji wa mapato stahiki kutokana na shughuli
za madini zinazofanyika katika sekta ikiwemo zile zinazokwenda sambamba na
sekta ya madini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko alimshukuru
mtoa mada kutokana na elimu ya takwimu aliyoitoa na kuahidi kuufanyia kazi
ushauri alioutoa.
Pia, ameitaka NBS kuendelea kutoa ushauri wa mara kwa mara wizara
lengo likiwa ni kuhakikisha sekta ya madini inachangia zaidi katika pato la
taifa.
0 comments:
Post a Comment