Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akitoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wakisikiliza ufafanuzi wa Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akitoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera Bi Costansia Buhiye akitoa neno kwa niaba wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoani humo mbele ya Waziri Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kutokana na ufafanuzi alioutoa kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Waziri Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akijadili jambo na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Kagera Mhe Oliver Semuguruka mara baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Na
Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera
Malalamiko ya muda mrefu ya
wakulima yaliyokuwepo kwamba ushirika unatoa bei ndogo, sasa yamepatiwa
muarobaini baada ya serikali kupitia kwa kina gharama za uendeshaji na
uongezaji thamani kwa zao la kahawa kwa Vyama vikuu vya ushirika Mkoani Kagera.
Serikali imepiga marufuku kwa
vyama hivyo vya ushirika kutoza zaidi ya shilingi 490 kwa kilo moja ya Kahawa
ya maganda kama gharama za uendeshaji na uongezaji thamani, Awali maainisho ya
gharama hizo yalikuwa ni makubwa ambapo kiasi cha shilingi 1350 kwa kilo moja
ya Kahawa ya maganda ilianishwa kama gharama za uendeshaji.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt
Charles Tizeba ameeleza agizo hilo Leo 12 Julai 2018 wakati akizungumza na
wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli
ya Bukoba Coop ambapo miongoni mwa ajenda ya kikao hicho ilikuwa ni kujadili
kuhusu soko la Kahawa na uendeshaji wa ushirika.
Dkt Tizeba amewaeleza wajumbe
hao kuwa amepiga marufuku hiyo kufuatia malalamiko ya wadau wa Kahawa Mkoani
Kagera ambapo gharama hizo zilionekana kuwa kubwa ukilinganisha na gharama
halisi.
"Ndugu zangu wajumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM inawezekanaje shilingi mia mbili inatozwa kama
ushuru wa chama kikuu, na shilingi mia mbili tena inatozwa kama ushuru wa chama
cha msingi, ni nani anaweza kukupa faida namna hii sasa rasmi ushuru huu
tumeupunguza kama nilivyoeleza" Alikaririwa Mhe Tizeba
Aliongeza kuwa swala la ushirika
ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo ni mkataba kati ya
wananchi na serikali katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015-2020 kwa
imani kubwa kwamba ndicho chombo pekee kitakacho mkwamua mkulima na changamoto
anazo kabiliana nazo kwenye Kilimo na masoko ikiwa ni pamoja na kujiondoa
katika umasikini.
Aidha, Dkt Tizeba aliwaeleza
wajumbe hao kuwa vyama vya ushirika havipaswi kuendeleza mazoea ya kujiwekea
gharama bila kwanza kutazama kipato cha mkulima huku akieleza kuwa amewaelekeza
wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambapo Wilaya zao zinalima Kahawa kote nchini
kufuatilia kwa karibu mwenendo wa masoko ya Kahawa kuanzia inavyokusanywa mpaka
wakati inapouzwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera Bi Costansia Buhiye amempongeza Waziri huyo
wa kilimo kwa kujibu kero namba 10 ya kikao cha Halmshauri kuu ya CCM kuhusu
wasiwasi wa bei ya kahawa na namna na uendeshaji wa ushirika.
Buhiye alimpongeza Waziri huyo
kwa kutatua kadhia mbalimbali za wakulima wa Kahawa katika ziara yake ya siku
tatu Mkoani humo huku akieleza kuwa ana imani kubwa sasa kuwa wajumbe hao
watatembea kifua mbele endapo wakulima wao watapatiwa bei nzuri.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment