Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe akitoa muhtasari wa uhalali wa uwepo wa OR-TAMISEMI na majukumu yake katika kikao cha mafunzo kwa kamati za kudumu za Bunge za Tawala za Mitaa,LAAC na PAC kilichofanyika leo katika ukumbi wa Msekwa, Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshighulikia afya Dokta Zainabu Chaula akiwasilisha mada kuhusu sekta ya afya katika kikao cha mafunzo kwa kamati za kudumu za Bunge za Tawala za Mitaa,LAAC na PAC kilichofanyika leo katika ukumbi wa Msekwa, Jijini Dodoma.
Baadhi ya maofisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakisikiliza mada katika kikao cha mafunzo kwa kamati za kudumu za Bunge za Tawala za Mitaa,LAAC na PAC kilichofanyika leo katika ukumbi wa Msekwa, Jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Tawala na Serikali za Mitaa wakisikiliza mada katika kikao cha mafunzo kwa kamati za kudumu za Bunge za Tawala za Mitaa,LAAC na PAC kilichofanyika leo katika ukumbi wa Msekwa, Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe. Tixon Nzunda akiwasilisha mada kuhusu sekta ya elimu nchini katika kikao cha mafunzo kwa kamati za kudumu za Bunge za Tawala za Mitaa,LAAC na PAC kilichofanyika leo katika ukumbi wa Msekwa, Jijini Dodoma.
............................................................
Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe amasema kuwa Sera ya Ugatuaji wa madaraka imeongeza uelewa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.
Ameyasema hayo wakati akitoa maelezo katika kikao cha mafunzo kwa kamati za kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali za Mitaa, Utawala na Serikali za Mitaa, na hesabu za Mashirika ya umma kilichoafanyika leo katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa, Jijini Dodoma.
Amesema kuwa karibu asilimia 90 ya vijiji na kata zinaandaa na kuwasilisha mipango shirikishi kwa wakati na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mipango kwa kutumia mfumo wa fursa za vikwazo katika ujenzi wa shule, vyumba vya madarasa, Ujenzi wa Zahanati, Vituo vya afya na miradi mingine ya maendeleo.
Mhandisi Iyombe amesema kuwa mpaka sasa Serikali inashule za sekondari za kata zipatazo 3,516 ambazo kwa sehemu kubwa zimejengwa kwa nguvu za wananchi ambapo nguvu hizi zimekuwa zikienda kasi wakati mwingine kutoendana nauwezo wa Serikali wa kuajiri wataalam, vifaa na na fedha za kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa na wananchi.
Anafafanua zaidi kuwa Serikali imeweza kuongeza mapato ya ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutokana na kuongezeka kwa vyanzo vya mapato, uwekezaji na kuimarika kwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato na matumizi. Pia mamlaka za Serikali za Mitaa zimeweza kupanga na kupitisha bajeti na kuibua vyanzo vya mapato.
Mhe Iyombe amesema kuwa dhana ya Ugatuaji wamadaraka kwa Umma inahusu kupeleka madaraka ya kisiasa kwa wananchi lengo likiwa ni kuwapa wananchi madaraka kupitia kwa viongozi wao wafanye maamuzi yanayohusu kuwapa wananchi uwezo wa kuamua , kupanga,kutekeleza na kutathmini mipango ya maendeleo kupitia wawakilishi wao, viongozi wa serikali za Mitaa kuanzia ngazi ya Kijiji na baraza la madiwani la Halmashauri.
Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshighulikia afya Dokta Zainabu Chaula amesema serikali imeweza kuboresha huduma za afya ambapo kwa mwaka 2007 idadi ya vituo vya afya ilikuwa 380 na kata zilikwa 2500 lakini mwaka 2017/2018 idadi ya kata ni 4,420 na vituo vya afya vimeongezeka hadi kufikia 535.
Amesema Serikali imejikita katika Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya afya nchini, kuajiri wataalam wa afya, uboreshaji wa takwimu kwa kutumia mfumo wa kielektroniki (GoTHOMIS), ukokotoaji wa mahitaji halisi ya dawa kwa mfumo mpya na kudhibiti makusanyo ya mapato katika vituo vya huduma pamoja na kuhimiza malipo ya kadi.
Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe. Tixon Nzunda amesema ugatuaji katika elimu hususani Elimu ya Msingi na baadae Elimu ya Sekondari ulitokana na Tamko la Rais la tarehe 12/02/2008 kuhusu kugatua Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari kutoka iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenda kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM). Kiutawala.
Aidha amesema ugatuaji wa elimu umewezesha kurahisisha Ongezeko la Wanafunzi wa Elimu za Msingi na Sekondari,Takwimu zinaonekana kuwa idadi ya wanafunzi wa Elimu ya Awali imeongezeka kutoka 851,084 (2009) hadi 1,436,322 (2017); Elimu ya Msingi kutoka wanafunzi 8,313,080 (2009) hadi 8,969,110 (2017); Elimu ya Sekondari kutoka wanafunzi 1,293,691 (2009) hadi 1,565,201 (2017).
0 comments:
Post a Comment