Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Peter Mavunde amewataka Wazazi na Jamii kutowafanya Watoto kama chanzo cha mapato kupitia Ajira na kubainisha kwamba Serikali haitasita kuwachukulia hatua wote watakaobainika kuwatumikisha watoto chini ya umri wa miaka 14.
“Watoto waha haki zao za kimsingi ambazo zinapaswa kulindwa na kamwe wasitumike kama mgongo wa kuingiza mapato.Watoto waache waishi na kutimiza ndoto za maisha yao kupitia Elimu na sio kutumikishwa kwa lengo la kupata ujira”Alisema Mavunde
Mavunde ameyasema hayo leo Jijini Mwanza katika kilele cha maadhimisho ya *SIKU YA KUPINGA AJIRA KWA WATOTO DUNIANI* ambapo ametumia fursa hiyo pia kuwataka wadau wa masuala ya Watoto kushirikiana na Serikali katika kutoa ELIMU kwa Jamii ili kutokomeza Ajira kwa watoto ifikapo Mwaka 2025.
Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya *WOTESAWA* Bi Angela Benedicto ameiomba Serikali kuzifanyia marekebisho mbalimbali sheria zinazomhusu mtoto ili kuondoa mkanganyiko katika utekelezaji wake.
0 comments:
Post a Comment