METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 1, 2018

MAVUNDE AWATAKA WATANZANIA KUJENGA UTAMADUNI WA KUNYWA MAZIWA

Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde  amehimiza jamii ya watanzania kutambua umuhimu wa maziwa kwa Afya ya mwanadamu kwa kujenga utamaduni wa kunywa maziwa kwa wingi kama inavyotakiwa na Shirika la Afya Duniani( *WHO* )kwamba mtu mmoja anatakiwa kunywa maziwa lita *200* kwa mwaka tofauti na ilivyo hivo sasa ambapo mtu mmoja wa Tanzania anakunywa wastani wa lita *47* kwa mwaka.

Mavunde ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati wa kilele cha wiki ya Unywaji maziwa leo ambapo alitumia nafasi hiyo  kugawa pakiti *30,000* za maziwa zilizotolewa na Kampuni ya *ASAS DAIRIES LTD* kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za Msingi za Jimbo la Dodoma Mjini na Wafungwa katika Magereza Dodoma.

Aidha Mavunde amechukua nafasi hiyo kuipongeza sana Kampuni ya *ASAS DAIRIES LTD* kwa namna ambavyo inashirikiana na jamii ya Watanzania  katika masuala mbalimbali ya kijamii na kuiomba kampuni hiyo kubuni bidhaa maalum itakayouzwa kwa bei ndogo  kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ili kuongeza idadi za lita za unywaji maziwa  kwa watanzania.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com