Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeandika historia mpya mara baada ya bajeti yake kuungwa mkono na waheshimiwa wabunge wote pasipo wabunge hao kuzuia shilingi kama ilivyokuwa siku za nyuma ikiwa ni wizara yenye kukosolewa na kila mbunge aliyesimama kuchangia hoja badala yake wabunge wamepongeza waziri na naibu waziri wa wizara hiyo pamoja na watendaji wao kwa mafanikio iliyoyapata na kuonyesha mwanga wa kufanya vizuri zaidi kwa kubaini mwarobaini wa kumaliza migogoro ya ardhi, kupanga miji na kusimamia mapatao yanayotokana na sekta hiyo.
Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Wizara hiyo imetenga kiasi cha fedha jumla ya shilingi 79 Bilioni na kupitishwa na kikao cha 40 cha Bunge la Bajeti chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe Mussa Azzan Zungu.
Aidha wakichangia wakati wa uwasilishwwaji wa bajeti hiyo wabunge tofauti tofauti mbali na kupongeza Waziri wa Wizara hiyo Mhe William Lukuvi na Naibu Waziri wake Mhe Dkt Angeline Mabula wametaja mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiwasumbua wananchi ambayo sasa mara baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo yataenda kupata suluhu ya kudumu wakitaja migogoro ya ardhi na upatikanaji wa hati.
0 comments:
Post a Comment