Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akitoa maelekezo leo wakati
alipotembelea kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya
ya Arusha kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akikagua baadhi ya majengo yaliyojengwa katika Kituo
cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuona
maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho
Jengo la Kituo cha afya cha Murriet
kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha , Jijini Arusha.
1 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akikagua baadhi ya mabati yaliyotumika katika ujenzi
wa Kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha
kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho
.......................................................................................................
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege
amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.Gabriel Fabian Daqorro kuhakikisha
anaunda timu ya wataalam kuchunguza ubora wa mabati yaliyotumika katika ujenzi wa
kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika kata ya Murriet Halmashauri ya jiji la Arusha
Ameyasema
hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa kituo cha Afya cha Murriet
kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimepatiwa shilingi milioni
750 kwa ajili ya ujenzi wa wa majengo ya wodi ya Wazazi, Maabara, chumba cha
upasuaji na chumba cha kuhifadhia maiti
Mhe
Kandege amemtaka kuhakikisha anachunguza
gharama za ujenzi wa majengo hasa jengo la kuhifadhia maiti kwa kuwa
gharama yake ni kubwa ikilinganishwa na ramani zilizotolewa na Serikali kwa nchi nzima kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo.
Amemtaka
Mkuu huyo wa Wilaya kuhakikisha wanafanya mapitio mapya ya makadiri ya ujenzi
yaliyofanyika katika jengo la kuhifadhia Maiti ambapo gharama iliyokadiriwa ni
shilingi milioni 51. Kwa jengo hilo.
“Sijaridhishwa
na makadirio ya ujenzi yaliyofanyika katika jengo la kuhifadhia maiti kwa kuwa
ramani hizo zimetolewa na Serikali nchi nzima kwa ajili ya ujenzi huo, hivyo
namtaka Mkuu wa Wilaya kufanya mapitio mapya ya makadirio ya ujenzi wa jengo
hilo.
Amesema
Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya
nchini hivyo inahitaji kuona thamani ya majengo yanayojengwa yanaenda sambamba
na fedha zilizotolewa na Serikali.
Mhe.
Kandege ameziagiza Halmashauri zote nchini kubana matumizi ili kiasi cha fedha
kitakachotolewa na Serikali kitumike kuongeza majengo mengine na kuimarisha
yaliyopo ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa jamii.
Ameelekeza
chumba cha kujifungulia akina mama wajawazito kitenganishwe kila kitanda ili
kuwa na usiri mama mjamzito anapojifungua.
Aidha
Mhe. Kandege ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Arusha kuhakikisha Ujenzi wa vituo
vya afya unakamilika kwa wakati ili wananchi wapate huduma za afya karibu na
maeneo wanavyoishi.
Wakati
huohuo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw. Athumani Kihamia amesema jumla ya shilingi milioni 700
zimepokelewa kwa ajili ya umaliziaji wa jengo la OPD pamoja na kujenga majengo ya wodi ya wazazi, Maabara,
chumba cha upasuaji na chumba cha kuifadhia maiti ambapo zaidi ya shilingi
milioni 462 zimetumika.
0 comments:
Post a Comment