Na
Bahati Mollel-TAA, Iringa
KLABU
ya michezo ya Uchukuzi iliyopo (Sekta ya Uchukuzi) imebuka kidedea katika
michezo ya michuano ya Kombe la Mei Mosi baada ya kushinda vikombe 13 vya
michezo 10 iliyoshindaniwa kwenye viwanja mbalimbali mkoani Iringa.
Timu
hiyo inayoundwa na wachezaji mahiri imeweza kutwaa ubingwa wa kwanza kwa
wanaume katika michezo ya mbio za baiskeli (Chaptele Muhumba), draft (Johanson
Ngido), bao (Said Omar) na kuvuta kamba, huku kwa wanawake wametwaa ubingwa
katika mbio za baiskeli na riadha (Scolastica Hasiri), bao (Sharifa Amir) na
draft olnel) na karata wanawake na wanaume (Zamatradi Yusufu na Mosses
Machunda).
Timu
ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imeshika nafasi ya pili kwa kujikusanyia
vikombe tisa kwa kutwa ubingwa wa soka, riadha wanaume (Lazaro Lugano) huku
ushindi wa pili katika michezo ya riadha wanawake (Cartace Manampo), na
baiskeli (Happy Mwanga), karata (Sheila Mwihava) na Nkwabi Kadago (mwanaume),
na ushindi wa tatu netiboli, Stanley Umbe (baiskeli) na Jackline Massawe (bao).
Timu
ya Chuo Kikuu cha Tiba ya Sayansi (MUHAS) wamekuwa watatu kwa kujikusanyia
vikombe vitano vya bingwa wa karata wanawake (Emily Kyando), ; mshindi wa pili
katika bao (Severina Mnyaga), huku mshindi wa tatu michezo ya kuvuta kamba na
baiskeli wanawake (Severina Mnyaga) na dratf (Rebecca Chaula).
Timu
ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameshika nafasi ya nne kwa kujikusanyia vikombe
vinne vya ushindi wa pili katika riadha, baiskeli na bao wanaume (Michael Luanga), Nehemiua Johnas na Suleiman Chitanda, huku
nafasi ya tatu ya draft ilichukuliwa na Joseph Mlimi.
Timu
ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAOT) wamejikusanyia vikombe vitatu
pekee na kuwa watatu. Vikombe vya ushindi wa pili draft wanawake na wanaume
Rosemary Skainde na Alphonce Sika na ushindi wa tatu wa kamba wanaume; nazo
timu za Ofisi ya Rais Ikulu, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Geita
Gold Mine (GGM) kila mmoja wamejikusanyia vikombe viwili, nazo timu za RAS
Iringa na Tumbaku ya Morogoro wote wamepata kikombe kimoja-kimoja.
Hatahivyo,
mgeni rasmi aliyefunga mashindano hayo yaliyoanza Aprili 17 mwaka huu,
Mwenyekiti wa TUICO Taifa, Paul Sangeze alisema ameshangazwa na kusikitishwa
kwa wanamichezo wafanyakazi kunyimwa fursa ya kuja kushiriki kwenye michezo hii
kwa visingizio mbalimbali, na anaungana na waandaaji kushangaa idadi kuwa ndogo
ya washiriki.
“Mashirikisho
yote ya wafanyakazi tumesikitika kwa idadi hii ndogo na tutahakikisha miaka
ijayo timu zinaongezeka zaidi, na tunaipongeza timu ya netiboli ya Ofisi ya
Rais Ikulu kushiriki wameonesha mfano mzuri,” amesema Bw. Sangeze.
Pia
amesema michezo mahala pa kazi inasaidia kujenga miili ya wafanyakazi na kuongeza
tija na bidii kazini kwani viongozi wasiopenda michezo wanasababisha wafanyakazi
kupata magonjwa nyemelezi.
Naye
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Mei Mosi, Bi. Joyce Benjamin alisema rais John
Pombe Magufuli hajawahi kukataza michezo, na inashangaza utashi wa viongozi wasiopenda
michezo wanaokataza timu zao kushiriki kwenye michezo.
“Tunaomba
viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa kila eneo la kazi kuingilia kati juu ya hili
katika dhana nzima ya wafanyakazi kufanya michezo na kushiriki kwenye michezo
ya mashirikisho mbalimbali kama Shimiwi, Shimuuta na kutofanya michezo
kunapingana na ilani ya Chama cha Mapinduzi, inayosema wazi juu ya kuinua
michezo nchini,” amesema Bi. Benjamin.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment