BMG Habari-Pamoja Daima!
Mwaka 2016 mradi wa “KUPANDA” ulianza kutekelezwa katika shule ya sekondari Idetemya iliyopo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza. Lengo la mradi huu ni kuboresha mazingira ya shule hususani kwa wanafunzi wa kike ili waweze kuhitimu na kufaulu masomo yao.
Mradi huu unatekelezwa na shirika la ASAP (Africa School Assistance Project) kutoka nchini Marekani, linalosaidia maendeleo ya elimu barani Afrika na katika shule hii ya sekondari Idetemya mradi umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike, nyumba ya mwalimu, vyoo pamoja na ukarabati wa madarasa.
Pia taasisi hii inatekeleza mradi wa kuboresha mazingira ya elimu katika shule ya msingi Bulolambeshi, Kata ya Idetemya wilayani Misungwi. Fuatilia makala hii fupi kufahamu zaidi namna taasisi hii inavyochangia uboreshaji wa sekta ya elimu nchini Tanzania.
Bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Idetemya wilayani Misungwi lililojengwa na taasisi ya ASAP kupitia mradi wa KUPANDA.
Choo cha kisasa kilichojengwa katika shule ya sekondari Idetenywa Misungwi.
Ukarabati wa madarasa katika shule ya sekondari Idetemywa uliofanywa na taasisi ya ASAP.
Nyumba ya mwalimu katika shule ya sekondari Idetemya iliyojengwa na taasisi ya ASAP.
Zaidi ya wanafunzi elfu moja wa shule ya msingi Bulolambeshi Kata ya Idetemya wilayani Misungwi wanategemea choo hiki. Taasisi ya ASAP imebaini kwamba hakikidhi mahitaji na sasa inajenga choo cha kisasa shuleni hapo.
Tayari ujenzi wa choo cha kisasa shule ya msingi Bulolambeshi umeanza.
Pia taasisi ya ASAP imekuwa ikiwasaidia kimasomo wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu, na hapa Mkurugenzi wa Miradi barani Afrika kutoka taasisi hiyo Zech Swett (wa tatu kushoto) ameitembelea familia ya mwanafunzi Evodia Anatory (wa pili kulia) katika Kijiji cha Mayolwa wilayani Misungwi. Anayezungumza ni mama mzazi wa Evodia.
Tazama HAPA Mabweni yaliyojengwa na taasisi ya ASAP katika shule ya Idetemya Misungwi.
0 comments:
Post a Comment