METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, May 13, 2018

SERIKALI YAFUTA LESENI ZOTE ZA KUHODHI KWENYE MADINI NA KUZIRUDISHA SERIKALINI


Tume ya Madini iliundwa kwa mujibu wa kifungu cha 21 cha Sheria ya Marekebisho Anuwai ya Sheria ya Madini Na. 7 ya Mwaka 2017. Mnamo tarehe 17 Aprili, 2018, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kulingana na Sheria tajwa, aliteua Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Madini. Ili kutekeleza majukumu yake, Tume ilifanya kikao chake cha kwanza tarehe 30 Aprili, 2018 Jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine, Tume iliazimia mambo  yafuatayo:

    i.        Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Madini zitakuwa Jijini  Dodoma katika Ofisi za Wizara ya Madini;
  ii.        Kuimarisha usimamizi wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na marekebisho yake ya Mwaka 2017 kwa lengo la kuhakikisha kuwa Serikali inamiliki hisa zisizopungua asilimia 16 ya mtaji wa Kampuni zinazomiliki migodi ya kati (MLs) na mikubwa (SMLs), Wazawa wanashirikishwa ipasavyo katika Miradi ya Madini na kunufaisha jamii katika maeneo ya migodi na  Taifa kwa ujumla;

iii.        Kuwajulisha wamiliki wote wa leseni zote za kuhodhi maeneo (Retention Licences – Jedwali Na. 1) kuwa leseni zao zimefutwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ikisomwa pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2017 na Kanuni ya 21 ya Kanuni za Madini (Haki Madini), 2018 Tangazo la Serikali Na.1/2018 na kwamba maeneo ya leseni hizo yamerudishwa Serikalini bila hakikisho la kupewa tena;

Jedwali Na. 1: Orodha ya leseni za kuhodhi maeneo zilizofutwa

Namba ya Leseni
Jina la Mmiliki
Aina ya Madini
Tarehe ya kutolewa
Tarehe ya kuisha muda
Ukubwa (Km2)
Mkoa/Wilaya
Hali halisi
RL 0001/2009
Kabanga Nickel Company Limited
Nickel
02/05/2009
01/05/2019
201.85
Kagera/ Ngara
Imefutwa
RL 0006/2009
National Mineral Development Corporation Limited
Gold
31/12/2009
30/12/2019
21.27
Shinyanga/ Kahama
Imefutwa
RL 0009/2014
Bafex Tanzania Limited
Silver, gold & Copper
01/09/2014
31/08/2019
12.58
Mbeya/ Chunya
Imefutwa
RL 0010/2014
Bafex Tanzania Limited
Silver, gold & Copper
01/09/2014
31/08/2019
12.59
Mbeya/ Chunya
Imefutwa
RL 0011/2014
Bafex Tanzania Limited
Silver, gold & Copper
01/09/2014
31/08/2019
11.83
Mbeya/ Chunya
Imefutwa
RL 0012/2014
Bafex Tanzania Limited
Silver, gold & Copper
24/09/2014
23/09/2019
11.27
Mbeya/ Chunya
Imefutwa
RL 0014/2014
Mabangu Mining Limited
Gold
31/10/2014
30/10/2019
2.94
Geita/Mbogwe
Imefutwa
RL 0015/2014
Resolute (Tanzania) Limited
Gold
31/10/2014
30/10/2019
0.91
Geita/Mbogwe
Imefutwa
RL 0016/2015
Wigu Hill Mining Company Limited
Rare Earth Elements
13/02/2015
12/02/2020
15.14
Morogoro
Imefutwa
RL 0017/2015
Nachingwea Nickel Limited
Nickel
21/04/2015
20/04/2020
48.8
Lindi /Nachingwea
Imefutwa
RL 0013/2014
Precious Metals Refinery Company Limited
Nickel
10/10/2014
09/10/2019
25.7
Simiyu/ Bariadi & Busega
Imefutwa


 iv.        Hadi kufikia tarehe 04/07/2017, kulikuwa na jumla ya maombi mapya ya leseni za uchimbaji wa kati (MLs) zipatazo 15 na ya kuhuisha 21. Pia maombi ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini (PMLs) yalikuwa 4,345 katika Ofisi za Madini za Mikoa na Wilaya kote nchini. Kadhalika, hadi kufikia tarehe 04/07/2017, kulikuwa na jumla ya maombi 240 ya leseni za utafutaji wa madini (PLs). Kati ya maombi hayo, 86 yalishalipiwa ada ya kuandalia leseni (preparation fee) na yaliyobaki hayajalipiwa. Kwa taarifa hii, waombaji wote wa leseni za madini wanatakiwa kukamilisha maombi yao ili yaendane na matakwa ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2017. Hii ni pamoja na:
·        Kulipia ada za kuandalia leseni za madini (PLs, PMLs, MLs na SMLs) kwa maombi yaliyokidhi vigezo vya kupewa leseni;
·        Kuwasilisha Local Content Plan kwa mujibu wa Vifungu vya 102, 103 na 104 vya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho Anuwai ya Sheria zilizoandikwa, Sheria   Na. 7 ya Mwaka 2017; kwa waombaji wa leseni za uchimbaji wa kati (MLs) na mkubwa (SMLs) wa madini;
·        Kuwasilisha Corporate Social Responsibility Plan; na tamko la Integrity Pledge kadri ya kifungu cha 105 na 106 kwa mtiririko huo wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2017 kwa waombaji wa leseni za uchimbaji wa kati (MLs) na mkubwa (SMLs) wa madini;
·        Waombaji wote wa leseni za utafutaji wa madini (PLs) kuwasilisha taarifa  za technical resources (Mine equipment, technical personnel,…) na Audited Financial Statements;
·        Waombaji wote wa leseni za uchimbaji wa kati (MLs) na mkubwa (SMLs) kuwasilisha Cheti cha Tathmini ya Athari za Mazingira (Environmental Impact AssessmentEIA Certificate), taarifa za Feasibility Studies, technical resources (Mine equipment, technical personnel,…), Audited Financial Statements, uthibitisho wa tathmini ya fidia na kutokuwepo kwa mgogoro/migogoro katika eneo linaloombewa leseni ya uchimbaji wa madini; na
·        Waombaji wote wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini (PMLs), baada ya kupata leseni na kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji, wawasilishe Mpango wa Uhifadhi wa Mazingira (Enviromental Protection Plan – EPP );

Nyaraka zote zinazotakiwa, ziidhinishwe na mamlaka zinazohusika na kuwasilishwa kwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini kupitia Sanduku la Posta 2292, DODOMA.



Imetolewa na:

Prof. Idris Kikula
MWENYEKITI
Mei 11, 2018

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com