METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, October 24, 2016

Watu wanne wauawa mjini Bangui

media
Raia wanne wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea katika mji wa Bangui ambapo mashirika ya kiraia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yalikua yalitoa wito wa kusalia nyumbani kwa ajili ya kuomba kuondoka kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo.

Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kinashtumiwa kushindwa kuyazima au kuyadhibiti makundi ya watu wenye silaha.

"Askari wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) waliingilia kati mapema Jumatatu hii katika mji wa Bangui ili kuondoa vizuizi vilivyokua vimewekwa barabarani na waandamanaji wanaowapinga," Minusca imebaini katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu hii jioni.

"Minusca inalaani kabisa matukio ambayo yaliathiri baadhi ya maeneo ya mji mkuu na inasikitishwa kuona hali hiyo imesababisha vifo vya raia wanne na kuwajeruhi wengine 14, ikiwa ni pamoja na askari watano wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, " taarifa hiyo imeongeza. Vurugu hizi "ni jaribio mpya la maadui wa amani kwa lengo la kuvuruga kurejea kwa hali ya kawaida ya kikatiba."

Minusca "pia inafutilia mbali kampeni ya kupakwa matope dhidi askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani na itaendelea na kazi yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Minusca pia inakumbusha kwamba vurugu zozote zile dhidi ya askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani zitapelekea wahusika kufunguliwa mashtaka katika mahakama za kimataifa," taarifa hiyo imehitimisha. 
RFI
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com