Waziri wa kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba
Na Bashiri Salum, Dodoma
Serikali imeagiza
sukari kiasi cha tani 70,354.35 kutoka nchi za nje lengo likiwa ni kujipanga
ili kuhakikisha kuwa hapatokei upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini.
Akizungumza na vyombo
vya habari hivi karibuni waziri wa
kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa tani 60,539.35 ya sukari itaanza kuingia hapa nchini katikati ya mwezi
Mei 2018 ambapo kiasi kilichobaki cha tani 9,815 kitaingia mwezi June mwaka 2018.
Aidha Dkt. Tizeba amefafanua kwamba hakutarajiwi
kuwa na upungufu wa sukari hapa nchini
kwa sababu hadi kufikia tarehe 10 mei 2018 katika maghala ya wazalishaji
na wafanyabiashara kulikuwa na tani 78,147.67
za sukari na kiasi kingine tani 25,441.25
kipo Bandarini .
Kwa kiasi cha sukari
ambacho tayari kipo hapa nchini kikijumlishwa na kiasi ambacho kitaingia hivi
karibuni kutoka nje ya nchi ni dhahiri kwamba nchi haiwezi kupata upungufu wa bidhaa hiyo,
alisema Mhe.Waziri.
Awali Dkt.Tizeba alisema kwamba mahitaji ya sukari nchi nzima
ni tani 630,000 ambapo kati ya hizo, tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya
viwandani na tani 485,000 ni kwajili ya matumizi ya kawaida.
Hata hivyo mapitio
yanaonesha kwamba msimu wa mwaka
2017/18 viwanda vya ndani vilizalisha tani
306,226 za sukari kwa matumizi ya
kawaida ambapo mwisho wa msimu huu
uzalishaji umefikia tani 307,481.76 aliongezea Dkt. Tizeba.
Akimalizia taarifa yake
Mhe. Tizeba amebainisha kuwa kwa kiasi ambacho sukari imeagizwa kutoka nje
Pamoja na viwanda vya ndani inadhihirisha kwamba hakutakuwa na upungufu wa aina
yeyote ya sukari hapa nchini na ikizingatiwa kuwa viwanda vitaanza uzalishaji mwingine
mwezi mei ambapo ukarabati (services ) itakuwa imekamilika .
0 comments:
Post a Comment