*Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli* leo amewasilisha mchango wake wa *Tsh 10,000,000* kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Veyula iliyopo Jijini Dodoma ikiwa ni ahadi aliyoitoa kwa wananchi wakati aliposimama kuwasilimia akitokea katika hafla ya Ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati.
Mchango huo umewasilishwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Deogratious Ndejembi ambaye pia amechangia *Tsh 1,000,000* kutimiza ahadi yake na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kuanza kuchimba Msingi wa ujenzi wa madarasa na kutumia fursa hiyo kuwataka watendaji wote kusimamia zoezi la ujenzi kwa ufanisi na kumwagiza **Lt Col Matina Mkuu wa Kikosi cha JKT Makutupora **kusimamia ukamilishwaji wa ujenzi wa madarasa hayo ndani ya wiki tatu.
Aidha,Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde **na DC Ndejembi waliungana na wananchi katika zoezi la uchimbaji msingi na baadaye Mh Mavunde alikabidhi kiasi cha *Tsh 5,000,000* mifuko ya Saruji *100* na kuahidi kuongeza *Tsh 5,000,000* ya ziada mapema wiki ijayo ikiwa ni mchango kutoka kwa marafiki wa Mbunge huyo,na pia alitumia fursa hiyo kumshukuru Mh Rais kwa kusaidia ujenzi wa madarasa hayo.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma **Ndg Godwin Kunambi **amewahakikishia wananchi kwamba Halmashauri ya Jiji la Dodoma italipia vifaa na gharama zote za kupaua madarasa hayo ikiwa ni sehemu ya mchango wa Jiji.
0 comments:
Post a Comment