METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, April 18, 2018

BILIONI 1.9 KUNUFAISHA WANAWAKE NA VIJANA WA MANISPAA YA UBUNGO

Hilo limebainika leo  makao makuu kibamba katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya  utaratibu mzima wa kupitishia pesa za mikopo ya wanawake,vijana kati ya Manispaa ya Ubungo na benki ya CRDB ambapo Mstahiki Meya,Mkurugenzi wa Manispaa na kaimu Mkurugenzi wa CRDB wamesaini mkataba huo.

Akiongea Mstahiki Meya Boniface Jacob amesema tayari manispaa ina pesa taslimu bil.1.9 ambazo zitatolewa kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu ambao wamekidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo baada ya mchakato wa kuwachuja,akiongelea kuhusu mustakabali wa zoezi hilo amesema zoezi hilo la utoaji mikopo ni endelevu.Na amewataka watakaonufaika kuzingatia masharti ya mikopo ili wengi zaidi wanufaike.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi John kayombo amesema jumla ya maombi yote katika upande wa pesa yalifikia bil 3 ambapo waliofahulu kupata baada ya mchujo watagharimu bil.2 na wote watapata kwani ni utaratibu wa manispaa kutenga kila mwezi asilimia kumi ya mapato yake kwa ajili ya mikopo ya vijana na kina mama ambayo ndio siri iliyopelekea Manispaa hii kuwa manispaa vya kwanza kutoa mkopo wa kiasi kikubwa ukilinganisha na Manispaa zingine Tanzania.

Aidha akiongelea tofauti ya mikopo inayotolewa Manispaa ya Ubungo na kwingine Kayombo amesema riba kwa wakopaji ni asilimia nane tu(8%) na sio asilimia kumi kama ilivyozoeleka.

Akiongelea  kuhusu wale ambao hawajafanikiwa kutokana na kutokidhi vigezo amesema Manispaa chini ya idara ya Maendeleo ya jamii watatoa mafunzo maalum kwao kwa ajili ya kuhakikisha wanakidhi vigezo ili waweze kupata mikopo hilo.

Nae kaimu Mkurugenzi wa CRDB alikuja katika hafla hii kwa niaba ya Mkurugenzi wa CRDB ndg.Charles Kimei amesema wanayo furaha kubwa kuona wamekuwa benki iliyochaguliwa kufanya kazi na Manispaa ya Ubungo na wameahidi kutoa ushirikiano na kutimiza yale yote waliyokubaliana katika mkataba,na wanajisikia fahari kufanya kazi na Manispaa hii kwani wameonyesha wako makini katika masuala mbalimbali.
Huu ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa wananchi.

Halmashauri ya manispaa ya Ubungo ina mwaka mmoja na miezi minne toka kuanzishwa lakini imekuwa manispaa ya kwanza kutoa kiasi kikubwa cha mkopo kwa wanawake na vijana.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com