METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 22, 2018

VYAMA VYA MSINGI VYATAKIWA KUTOA MIKATABA KWA MAKATIBU WAKE

Serikali wilayani Nachingwea mkoani Lindi imeviagiza vyama vya msingi kuhakikisha inawapatia mikataba ya kisheria makatibu wa vyama hivyo ili kuwawezesha Kupata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kulipwa mishahara kwa wakati, sambamba na kuwataka wajiepushe kuhujumu fedha za wakulima wa zao la Korosho.

Akizungumza katika zoezi la kufunga mafunzo ya siku Tatu kwa makatibu hao kutoka wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Liwale juu ya namna ya kutunza nyaraka na uandishi wa vitabu vya kumbukumbu, mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Mh. Rukia Muwango, amesema sambamba na hilo, mikataba hiyo inatakiwa iwekwe kipengele kinachomtaka mwajiriwa kuorodhesha mali anazozimiliki.

"Kwasababu watendaji wengi kwenye vyama vya msingi wamekuwa wakifanya kazi bila ya kuwa na mikataba ya kisheria na hiyo inawafanya wao kuweza kufanya ubadhirifu kwenye vyama hivi vya msingi na hatimae wanaviletea hasara, lakini kuwakosesha wakulima haki zao.."

"kwahiyo tumeelekeza viongozi wote wa vyama vya msingi watoe mikataba ili watendaji hawa wafanye kazi kulingana na mkataba unavyoolekeza, na mikataba hiyo iwe ya kisheria inayoelekeza haki na wajibu."

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com