METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, January 7, 2018

MBUNGE WA ILEMELA AFANYA ZIARA SOKO LA MWALONI KIRUMBA KUSIKILIZA KERO NA CHANGAMOTO

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amefanya ziara kwa kutembelea na kusikiliza wafanya biashara wa soko la samaki la Mwaloni Kirumba juu ya kero na changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi

Akizungumza na wafanya biashara hao Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kuelezea juu ya mikakati na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli katika kuhakikisha wafanya biashara hao wanakuwa na mazingira mazuri na bora ya kibiashara sokoni hapo amewahakikishia ushirikiano kama Mbunge wa Jimbo lao huku akimtaka mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya watumishi wa serikali wanaohujumu wafanyabiashara wa sokoni hapo

‘… Ndugu mkurugenzi nakuomba utakapoondoka hapa uondoke na watumishi hawa wanaotuhumiwa kukwamisha shughuli za maendeleo za wafanyabiashara hawa ili uchunguzi uweze kufanyika …’ Alisema

Akimkaribisha mbunge wa Jimbo hilo, Mwenyekiti wa soko mbali na kuwataka wafanya biashara kuwa wawazi kwa kuelezea changamoto zinazowakabili amemshukuru Dkt Angeline Mabula kwa uamuzi wake wa kuamua kulitembelea soko na kuzungumza na wafanyabiashara hao

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela Ndugu John Wanga amemuhakikishia Mbunge huyo kuwa atahakikisha watumishi hao wanaokwenda kinyume na taratibu za utumishi wa Umma sokoni hapo wanachukuliwa hatua kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma huku akiasa ushirikiano wa pamoja katika kuhakikisha wanajiletea maendeleo

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
07.01.2018

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com