Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mhe Dkt Angeline Mabula ametua mkoani Tanga kwa muendelezo wa ziara yake yenye lengo la kukagua ukusanyaji wa kodi za ardhi, utunzaji wa kumbukumbu za ardhi na utatuzi wa migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi , Ambapo akiwa wilaya ya Korogwe mkoani humo amewataka wataalamu wa ardhi kuwa waadilifu kwa kufuata sheria na taratibu za ardhi ili kuepusha migogoro kwa wananchi huku akisisitiza juu ya kuwatendea haki wananchi kwa kuitafutia ufumbuzi wa haraka migogoro yote iliyowasilishwa kwao na kusisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli haimvumilia mtumishi yeyote anaezalisha migogoro ya ardhi isiyo ya lazima kwa wananchi
“… Kama ikitokea hichi mlichokisema si cha kweli wewe ulietoa taarifa ujiandae kuwajibika, Kwa sababu hatuwezi kukubali kila siku wananchi wanateseka, Na wawakilishi wa wananchi wanalalamikia hili jambo na nyie mpo, Sasa nnachosema kesho nendeni kwenye eneo la mgogoro itisheni mkutano na kabla sijarudi Dar es salaama muhakikishe naipata taarifa ya utatuzi wake …” Alisema
Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula pia amewataka watumishi wa kada ya ardhi kuhakikisha wanaongeza kasi na umakini wa ukusanyaji wa kodi za ardhi ili kuongeza mapato ya Serikali yatakayotumika katika shughuli mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo
Kwa upande wao viongozi wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga kwa pamoja wamemshukuru Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula kwa uamuzi wake wa kufika katika wilaya yao, kusikiliza kero na changamoto za ardhi zilizokuwa zikiwakabili wananchi wa wilaya hiyo na kukaa kwa muda mrefu bila ufumbuzi wa uhakika
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
03.03.2018
0 comments:
Post a Comment