Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ameitembelea mipaka ya Tanzania ya Namanga, Horohoro na Horiri kwa wakati tofauti alipokuwa akifanya ziara ya utatuzi wa migogogro ya ardhi, ufuatiliaji wa makusanyo ya kodi za ardhi na utunzaji wa kumbukumbu za ardhi kwa mikoa ya Mara, Kilimanjaro na Arusha kabla ya kuendelea na ziara yake mkoani Tanga
Aidha Naibu Waziri huyo alipata fursa ya kukagua vigingi vya mipaka ya ardhi baina ya nchi ya Tanzania na Kenya huku akiiasa Jamii kutoa ushirikiano katika kutunza alama hizo za mipaka ya kisheria na kurudishia alama zote zilizoanza kupotea katika kijiji cha mahandakini, kitongoji cha Jasini, wilaya ya Mkinga
Katika ziara hiyo Mhe Dkt Angeline Mabula pia amepata fursa ya kuzungumza na idara za ardhi za wilaya na mikoa hiyo, kufanya mikutano na wananchi ya kusikiliza kero na changamoto za ardhi na kisha kuzipatia ufumbuzi huku akishuhudia tukio la tofauti kwa nyumba moja kuwa na Sebule nchini Tanzania na Chumba kuwa nchini Kenya
Ikumbukwe kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi anaendelea na ziara yake mikoa mbalimbali nchini
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
03.03.2018
0 comments:
Post a Comment