Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi kombe kampteni wa timu ya Iringa United baada ya kuwafunga Mtwivila City kwa njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana goli moja moja
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na
mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi zawadi ya jezi
kampteni wa timu ya Mtwivila baada ya kuwafungwa na timu ya Iringa United kwa
njia ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa
wamefungana goli moja moja
mashabiki na viongozi wa timu ya Iringa United wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga timu ngumu ya Mtwivila City kwa njia ya mikuju ya penati na kuwa wawakilishi wa mkoa wa Iringa kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na
mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi pesa na zawadi mchezaji bora wa mashindano Razack Kibuga ambaye ametoka katika timu ya Iringa United United
Baadhi ya wadau na mpira wa mikuu mkoani Iringa wakiwa wapo sambamba na kiongozi wa Iringa United walipokuwa wakifuatilia kwa ukaribu mechi katika ya Iringa United na Mtwivila City kutoka kushoto anaitwa Frank Lyimo kutoka kituo cha TV cha IMTV ,Ally Msigwa ambanye ni mkurugezi mtendaji wa Iringa Football Academy na anayefuata ni Steve Lihawa mtangazaji wa kipindi cha michezo cha radio Ebony fm iliyopo mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
TIMU ya
Soka ya Iringa United imefanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya Mkoa wa Iringa
baada ya kuibuka na ushindi penati 3 - 1 dhidi ya Mtwivila Fc.
Katika
mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Samora timu ya Mtwivila Fc walikuwa wa
kwanza kupata bao dk 8 kupitia kwa mshambuliaji hatari David Mwanga baada
uzembe wa golikipa wa Iringa United Nelly Mkakilwa kuponyokwa na mpira na
kumpita tobo.
Mchezo
huo uliokuwa wa kukamiana mwanzo mwisho huku baadhi ya wachezaji wakionyesha
ufundi mwingi wa kuchezea mpira hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mtwivila
walikuwa wakiongoza bao 1.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi kwa kila timu kutaka kuonyesha kuwa hawajabahatisha
kufika fainali ya ligi ya Mkoa kwa Mtwivila wakitaka kuongeza huku Iringa
wakitaka kurudisha.
Mchezaji
bora wa mechi ya nusu fainali Razack Kibuga aliibuka shujaa baada ya
kusawazisha goli katika dk 76 na kuwaacha wachezaji wa Mtwivila wakilaumiana.
Mara ya
dakika 90 kumalizika ndipo hatua za kupigiana matuta ilipowadia ambapo timu ya
Mtwivila fc ilikosa penati 3 na Iringa United kupata penati 3 dhidi ya 1.
Kutokana
na ushindi huo timu ya Iringa United imejinyakulia jezi seti moja, mipira
miwili huku timu ya Mtwivila wakiondoka na jezi na mpira mmoja.
Mchezaji
bora wa mashindano hayo aliibuka Razack Kibuga wa Iringa United aliyeondoka na
zawadi ya sh.100,000 na cheti golikipa bora alikuwa Nelly Mkakilwa toka Iringa
United aliyepata sh.50000
Katika
mchezo huo mgeni rasmi alikuwa mfanyabiashara maarufu na mdau mkubwa wa soka
Mkoani hapa Feisal Abri Asas ambaye alikabidhi kombe la ubingwa kwa nahodha wa
Iringa united, Ahmed Kivike.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi kombe hilo Feisal alisema kuwa anatarajia kudhamini ligi ya
Mkoa mwakani kwa kuwa mwaka huu yamekuwa na mafanikio makubwa.
Wakati
huo huo ya soka ya Mkimbizi fc imefanikiwa kushika nafasi ya tatu ya ligi ya
mkoa baada ya kuwafunga timu ya soka ya Mshindo fc mabao 5 - 4.
Katika
mchezo huo mkali uliopigwa majira ya saa nane mchana katika uwanja wa Samora
timu ya Mshindo 'wabishi wa mjini' itabidi wajilaumu kwa kuwa hadi kipindi cha
kwanza walikuwa wanaongoza goli 3 - 2 kwa magoli yaliyofungwa na Michael Chader
dk za 8,17 na 23.
Magoli
ya Mkimbizi fc yalifungwa na Said Kaliumi aliyefunga magoli matatu katika dk za
10 na 29 na 53.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi kwa Mshindo Fc kufunga goli la nne kupitia Michael
Chader katika dk 50 lililodumu hadi dk ya 53 ambapo Mkimbizi Fc walijipatia
goli kupitia kwa Said Kaliumi.
Mkimbizi
Fc wakiwa nyuma kwa goli mbili walikuja kwa kasi na kuanza kufunga katika
dk za 64 na 70 na kufanya matokeo kuwa 5 - 4
Kwa
ushindi timu ya mkimbizi imefanikiwa kuwa Mshindi wa tatu katika ligi ya Mkoa
na kuondoka na zawadi ya jezi seti moja.
0 comments:
Post a Comment