WAZIRI wa Mambo ya ndani na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi Dk
Mwigulu Nchemba akipata maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa vinavyotumika
kwenye maabara za sayansi katika shule ya sekondari Lulumba alipokwenda jana
kuongoza harambee ya ukarabati wa madarasa na ofisi za mwalimu na ujenzi wa
mabweni ya shule hiyo iliyopo wilaya ya Iramba mkoa wa singida.
WAZIRI wa Mambo ya ndani na mbunge wa jimbo la
Iramba magharibi Dk Mwigulu Nchemba
(katikati) akiangalia wanafunzi wa kidato cha tatu mchupuo wa sayansi wa shule
ya sekondari ya Lulumba wakichanganya kemikali kuunda gesi, alipokwenda jana
kuongoza harambee ya ukarabati wa madarasa na ofisi za mwalimu na ujenzi wa
mabweni ya shule hiyo iliyopo wilaya ya Iramba mkoa wa singida.
WAZIRI wa Mambo ya ndani na mbunge wa jimbo la
Iramba magharibi Dk Mwigulu Nchemba (katikati) akikata utepe kuashiria
kuanza kwa harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ukarabati wa madarasa,
ofisi za mwalimu na ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari Lulumba iliyopo
wilaya ya Iramba mkoa wa singida.
WAZIRI wa Mambo ya ndani, Dk Mwigulu Nchemba amewataka
walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema
na inapobidi matumizi ya fimbo yatumike.
Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya
Sekondari Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida, jana, Dk Nchemba
alisema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi ili kutengeneza
hatma ya nchi.
"Kuna wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi lakini
ninyi hamuoni hii na kulalamika tu, kinachofanyika ni kwa manufaa
yetu...niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo
fanyeni hivyo ili kutengeneza taswira ya nchi yetu," alisema Dk Mwigulu.
Alisisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa
kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa.
Alisema ni majengo ya taasisi yanapaswa kuwa bora zaidi na sio
kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo
yaliyopo.
"Naunga mkono ujenzi huu wa mabweni ya wanafunzi, ukarabati
wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu hivyo nachangia mifuko 200 ya saruji
nawaahidi pia kutoa Sh milioni sita," alieleza.
Mkuu wa Wilaya Iramba, Emmanuel Luhaula alisema shule higo
imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma kutokana na umahiri wa walimu kwani watoto
hao wanajua kujieleza kama vile wanasoma chuo kikuu.
Alisema wananchi wa Iramba wanatakiwa kujivunia kuwa na
shule zao pamoja na walimu hao ili kuboresha elimu wilayani humo.
"Unafanya jitihada ili kuhakikisha kila sekondari
kunajengwa mabweni ili kuondoa kero za wanafunzi.Sisi wa Iramba tushindwe wenyewe
kukutumia. Nimekuwa Mbunge lakini anayoyafanya mbunge huyu Mimi
sikuyafanya," alisema Luhaula.
Naye, Mkuu wa shule hiyo, Jeremiah Kitiku alisema licha ya
kufanya vizuri kitaaluma, wanakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa baadhi ya
majengo, upungufu vitabu vya masomo ya kiada 274.
"Mahitaji ya vitabu vya kiada no 2,802 vilivyopo 2,328
upungufu ni 274. Pia tunachangamoto ya kutokuwa na uzio kwa usalama wa
wanafunzi, walimu na mali za shule," alisema Kitiku
Hata hivyo, alisema malengo ya shule hiyo ni ukarabati wa vyumba
tisa vya madarasa na ofisi za nane za walimu ambazo zitagharimu Sh
Milioni 169.4.
Katika harambee hiyo, saruji iliyokusanywa ni mifuko 209, ahadi
ya fedha ni 8,486,000, ahadi ya mifuko ya saruji 572, Gypsum 50 na
nondo tani moja jumla ya ahadi na fedha taslimu ni 19,494,300
Mwisho
0 comments:
Post a Comment