Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki
akisisistiza jambo kwa uongozi wa kiwanda cha kutengeneza Saruji cha
Dangote kilichopo Mkoa Mtwara alipotembela kukagua na kusikiliza
changamoto za wawekezaji mkoani humo.Katikati ni Mtendaji Mkuu wa
kiwanda hicho Bw.Jagat Rathee.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki
akioneshwa namna mfumo wa TEHEMA unavyorahisisha utendaji kiwandani hapo
na Mhandisi Brezil Omary wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
Sehemu ya wajumbe waliposhiriki
katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki wakati wa ziara yake katika
kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Sekta ya Uzalishaji Balozi Celestine Mushi akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
Viwango wa Kiwanda cha
kutengeneza saruji cha Dangote Bw. Issawema akiwaonesha Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah
Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt.Angeline Mabula matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kuendesha
kiwanda hicho.
…………………………………………………….
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki ametoa
muda wa wiki moja kwa Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote
kuwasilisha taarifa ya utendaji ambazo kwa zaidi ya miaka miaka mitatu
hawajaziwasilisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama sheria na
taratibu za nchi zinavyoelekeza.
Waziri Kairuki ambaye aliongozana
na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline
Mabula Katika ziara yake ya kutembelea, kukagua maeneo mbalimbali ya
uwekezaji na kuongea na wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Lindi
septemba 27,2019 ameuelekeza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kila
baada ya miezi sita wanawasilisha taarifa za kiutendaji TIC.
Waziri Kairuki aliwaeleza
masikitiko yake viongozi wa kiwanda hicho kwa kutowasilisha taarifa za
utekelezaji wao ikiwemo zinazohusu historia ya mradi, mipango ya
upanuzi, kodi wanazolipa, faida pamoja na changamoto wanazokabiliana
nazo na ushauri wao.
“Nimesikitishwa sana na suala
hili la kutopeleka taarifa zenu TIC ambapo inafahamika suala hilo ni la
kisheria na lazima litekelezwe kwa wakati,hivyo kuanzia sasa nimewapa
wiki moja mhakikishe taarifa hizo zinawasilishwa haraka,”alisisitiza
Waziri Kairuki.
Aidha amewapongeza Dangote kwa
uwekezaji huo mkubwa pamoja na kuanza ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme
wao wenyewe megawati 25 ambao megawati 5 zitaingia kwenye gridi ya
taifa.
Amewataka wawekeze na maeneo
mengine siyo kwenye saruji tu na kuagiza TIC kupitia mikataba ya
utendaji ya wawekezaji wote mahiri kuona ni wapi wanaweza kuwekeza
zaidi.
Wakiwa Mkoani Lindi Waziri
Kairuki na Mhe. Mabula walitembelea mgodi wa madini ya uno (graphite)
uliopo katika Kijiji cha Matambalale Kusini Wilaya ya Ruangwamkoani
Lindi na kuona shughuli za awali za mradi huo ambapo Meneja wa kampuni
ya Lindi Jumbo inayochimba madini hayo Bw Paul Shauri amesema mgodi
utajengwa kwa muda wa miezi tisa na wanatarajia kuwekeza zaidi ya dola
za kimarekani milioni 30.
Akiongea mgodini hapo Dkt.Mabula
ameziagiza Halmashairi zote vijiji vyenye maeneo ya uwekezaji kufanya
zoezi la kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi watenge maeneo ya uwekezaji
wayahaulishe yawe mali ya kijiji ili mwekezaji akipatikana watimize
masharti mengine tu.
“Hakuna sababu ya mwekezaji
kuanza kuhangaika na mambo madogo kama hayo ambayo yanampotezea wakati
ni lazima halmashauri zijipange ili kumwekea mwekezaji mazingira mazuri
avutiwe kuwekeza”alisema Dkt.Mabula
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Ruangwa Hashim Mgandilwa akiwakaribisha Mawaziri hao amesema Serikali
ione kuna sababu ya kuharakisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara
za wilaya hiyo kwani kuna makampuni mengi makubwa yameonesha nia ya
kuwekeza.
Amesema wilaya hiyo pia
inakabiliwa na changamoto ya mipaka ya asili na kwamba suala hilo tayari
linaendelea kutatuliwa kwa viongozi na watendaji kutoa elimu kwa
wananchi.
0 comments:
Post a Comment