Kampeni ya kufichua watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi imezinduliwa rasmi Nachingwea tarehe 24 /3 /2018
Madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), wameikagua hospitali ya wilaya ya Nachingwea na kuona Chumba cha upasuaji kinakidhi kufanikisha malengo baada ya kufanyiwa maboresho ambayo wametoa maelekezo kwa Uongozi wa Wilaya, wao watakuja na vifaa vyote vinavyohusiana na Matibabu ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Tayari tuna orodha ya watoto wenye matatizo hayo kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Lindi na tunaendelea kuwapokea hadi Tar 10 /4 /2018, ambapo ndani kipindi cha Mwezi Aprili watarudi kwaajili ya zoezi la upasuaji na kutoa ushauri wa kitabibu kwa. Wananchi wa Mikoa ya Kusini changamkieni Fursa Adimu hii.
0 comments:
Post a Comment