14 March 2018
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole asubuhi hii ametembelea mradi wa Serikali wa Bwawa la ufugaji wa Samaki uliopo katika Kata ya Biturana Kijiji cha Biturana, Wilayani Kibondo.
Baada ya kujionea mradi huo wa Bwawa la Samaki katika Kata ya Biturana uliyoanzishwa februari 2017 Mwaka jana kama sehemu ya mpango wa serikali wa kunusuru kaya maskini kisha kuwasilikiza wananchi, wanachama wa CCM na Viongozi.
Ndg. Polepole amegundua kuwa mradi huo wa Samaki hadi leo hii March Mwaka 2018 haujawanufaisha wananchi waliokusudiwa hata kidogo ikiwa ni pamoja na kuvua Samaki ama kupata fedha yoyote.
Ndg. Polepole ameelekeza Serikali ya Wilaya ya Kibondo kuwachukulia hatua za kinidhamu watendaji wote wa serikali waliohusika katika ubadhirifu wa mradi huo wa Serikali kwa wananchi.
"Hawa ni maskini wamegeuzwa vibarua, hii ni kinyume kabisa na misingi na imani ya Chama chetu na Serikali ya CCM lengo lake nikuwasaidia wananchi kuondokana na umaskini ili waweze kujitegemea". amesema Ndg. Polepole
Akipokea maelekezo hayo Ndg. Loius Peter Burra Mkuu wa Wilaya ya Kibondo amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo amsimamishe kazi Mtendaji wa Kata ya Biturana na maafisa wote wa serikali waliohusika na mradi huo ili kupisha uchunguzi wa jambo hilo chini ya tume maalumu itakayoundwa kuchunguza ubadhirifu huo.
Huu ni muendeleo wa ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020 kwa vitendo.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
0 comments:
Post a Comment