Tofali zaidi ya Elfu Hamsini na mbili na mia tano zimefatuliwa na kusambazwa katika kata mbalimbali za Jimbo la Ilemela kupitia taasisi ya The Angeline Foundation ili kutekeleza miradi mipya ya maendeleo na kuifanyia ukarabati miradi ya zamani ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi
Akizungumza kwa wakati tofauti Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ndie muasisi wa taasisi hiyo Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi wake ikizingatiwa kwamba Serikali peke yake bila wadau wengine haiwezi kufanikisha kila kitu na kueleza juu ya miradi iliyokwisha fanikiwa kupitia tofali zilizofatuliwa na taasisi hiyo ikiwemo ujenzi wa maboma ya vyumba 28 vya madarasa kati yake 22 yamekamilika huku 6 yakiendelea kujengwa, ujenzi wa vyoo 3, Zahanati 3 zinazoendelea kujengwa, Ofisi 2 za Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya yake ya Umoja wa Vijana UVCCM zinazoendelea kujengwa, huku akiwataka viongozi na wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kufanikisha shughuli za maendeleo ndani ya Jimbo hilo
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyamhongolo Mhe Andrea Nginila akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika kikao cha baraza la madiwani cha upokeaji wa taarifa za kata amemshukuru mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula kwa kuanzisha mradi huo uliosaidia ujenzi wa zahanati yake ya Nyamhongolo, Ujenzi wa ofisi ya mtaa na madarasa huku akimhakikishia ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo
Nae Diwani wa kata ya Buzuruga Mhe Richard Machemba mara baada ya kuwasilisha taarifa yake pia amemshukuru mbunge huyo huku akiongeza kuwa suala la maendeleo halina itikadi ya chama nakumuomba kuendelea kuungana pamoja katika kuwatumikia wananchi wa kata yake huku Diwani wa Kata ya Nyasaka Mhe Shaban Maganga pia akishukuru kwa ufanikishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya kata yake kupitia tofali hizo zilizotolewa na mhe mbunge wa jimbo hilo
Akihitimisha Mstahiki meya wa manispaa hiyo Mhe Renatus Mulunga na mkurugenzi wake John Wanga nao mbali na kupongeza juhudi za mbunge huyo wametaka kuungwa mkono na kumtia nguvu huku diwani wa viti maalumu kupitia CCM Mhe Denisa Pagula akiunga mkono pia jitihada hizo
Mradi huo wa tofali mpaka sasa umenufaisha zahanati za Buzuruga, Nyamhongolo, Nyamwilolelwa, Kirumba na Kahama, Na shule ya msingi Kitangiri, shule ya msingi Nyasaka, Shule ya msingi Nyambiti, Shule ya msingi Igombe, Shule ya msingi Buhilya, Shule ya msingi Isenga, Shule ya Sekondari Bujingwa, Shule ya Sekondari Nyasaka
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
14.03.2018
0 comments:
Post a Comment