Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita akizungumza na waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wakati wa ibada, leo 3 Machi 2017. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe akizungumza wakati wa ibada mara baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, leo 3 Machi 2017.
Waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe akizungumza wakati wa ibada mara baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, leo 3 Machi 2017.
Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita akikabidhiwa kitabu cha Pendo lisilo kifani kilichoandikwa na Ellen G. White mara baada ya kuzungumza na waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe wakati wa ibada, leo 3 Machi 2017.
Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita akifanyiwa maombi na mchungaji Lazaro Mbogo wa kanisa la waadventisti Wasabato Maganzo kwa ajili ya utendaji uliotukuka kwa kusimamia haki na wajibu mara baada ya kuzungumza na waumini wa kanisa la Waadventisti Wasabato katika Kijiji na Jimbo la Bukombe wakati wa ibada, leo 3 Machi 2017.
Na Mathias Canal, Geita
Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni
Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita amefanikisha upatinaji wa jumla ya
shilingi milioni 4.6 kwa ajili ya ununuzi Wa Vifaa vya muziki kwa ajili ya
kwaya ya Maganzo katika kanisa la Waadventisti Wasabato.
Mhe Biteko ameendesha harambee hiyo 4 Machi 2018 katika ibada ya
kawaida ya juma kwa mujibu wa utaratibu wa kanisa hilo aliposhiriki ibada
maalumu ambapo pamoja na mambo mengine waumini wa kanisa hilo walimuomba
kuchangia ununuzi Wa Vifaa vya kwaya hiyo kwa ajili ya kuendeleza utumishi wa
kuhubiri injili kwa njia ya uimbaji.
Katika harambee hiyo Mhe Biteko alichangia shilingi milioni 2
papo hapo huku akitumia nafasi hiyo kuendesha harambee ambayo ilipelekea
kupatikana shilingi milioni 2.6 hivyo kupelekea kwaya hiyo kupata jumla ya
shilingi milioni 4.6 huku uhitaji wa ununuzi wa Vifaa hivyo vya muziki nukiwa
ni shilingi milioni 10.
Akihutubia mamia ya waumini hao Mara baada ya kupewa nafasi ya
kuwasalimia waumini Wa kanisa hilo Mhe Biteko alisisitiza kuwa wananchi kwa
ujumla wake wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano
inayooongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe
Magufuli kwani imejipambanua kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali zao.
Aliongeza kuwa katika sekta ya Madini ambapo ndiyo Wizara
aliyopewa jukumu ya kuiongoza Mhe Biteko alisisitiza kuwa Rais Magufuli
amedhamiria kurejesha uchumi fungamanishi kwa wananchi hususani kuwainua kwa
kuwalea wachimba wadogo hatimaye kufikia uchimbaji wa kati na hatimaye baadae
kuwa wachimbaji wakubwa.
Aliwasihi waumini hao kuiombea serikali ya Rais Magufuli
sambamba na wateule na watumishi wake wote ili waendelee kuliongoza Taifa na
sekta mbalimbali katika ushirika mwema wakiongozwa na roho mtakatifu kila mmoja
kwa imani yake.
Alisema kufanya hivyo ni kulinufaisha Taifa kwani watendaji
wengi wanafanya kazi kwa weledi lakini majukumu hayo yamekuwa na lawama nyingi
kwani usimamizi wa sheria hauwezi kumfurahisha kila mtu lakini Taifa lolote ili
liendelee ni lazima kuwe na usimamizi madhubuti wa sheria na taratibu za nchi.
Alisema kuwa wananchi wa Tanzania wamezaliwa katika nchi ambayo
inautajiri wa kila aina kwa kuwa na Rasilimali nyingi yakiwemo Madini mengi
lakini ilisalia kuwa nchi nufaishi kwa wageni kuliko wazawa.
Hivyo utashi wa serikali ya awamu ya tano ni kuwainua wananchi
wanyonge ambao kwa muda mwingi walipoteza matumaini katika kipindi kirefu
pasina fikra za mafanikio.
Naibu Waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko leo 4 Machi 2018
ameanza ziara ya siku nne katika Jimbo lake la Uchaguzi (Bukombe) Mkoani Geita
itakayofika ukomo 6 Machi 2018 ambapo pamoja na mambo mengine
atakutana na wapiga kura wake ili kusikiliza matatizo yanayowakabili ikiwa ni
pamoja na kuyatafutia ufumbuzi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment