Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba ametembelea kukagua ujenzi wa nyumba za polisi wilaya ya Arusha ambazo ziliungua kwa ajali ya moto uliyotokea mwaka jana umefikiaje mpaka sasa na kuridhika na hatua iliyofikia.
Dkt mwigulu amesema aridhika na hatua iliyofikia ya ujenzi wa nyumba za askari polisi ambazo ni za kisasa kabisa na kupongeza hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli kusaidia fedha ili ujenzi huu uanze mala moja, pia mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na wafanyabiashara wa Arusha kusaidia ujenzi wa nyumba hizo mpaka sasa ulipo kamilika kwani walichukua hatua mapema tupale moto ulipotokea.
"Leo hii mmeona nyumba hizi za kisasa ambazo zitafanya askari wangu kuanza kupigia selfie katika nyumba zao kwamba hapa ndipo ninapokaa, ili ni jambo kama waziri na mshukuru sana Rais na litaongeza morali ya kuendelea kufanya kazi nzuri wanayoifanya" Waziri Mwigulup
Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemshukuru waziri Mwigulu kwa msaada wake wa kufanikisha ujenzi huo unafanukiwa na kufikia hapo kwani kama waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani amekua karibu nao sana na kukagua kila hatua inayofikiwa.
RC Gambo ameongeza kusema kuwa kwasasa wamemuomba waziri Mwigulu awasaidie gari la polisi katika kituo cha polisi murieti na amekubali kuwasaidia kuwaletea gari ili kusaidia kupunguza matukio ya kiharifu maeneo hayo kwani kwasasa mji huo watu wengi wanaishi maeneo hayo na askari wanategemea gari linalotoka kituo kikuu cha polisi Arusha.
0 comments:
Post a Comment