Wazee
wa kimila katika kijiji cha Maguruwe kata ya Bunduki wakimsimika na kumpa
heshima maalum Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.
Wakazi
wa Maguruwe wakimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa
Maguruwe Wilayani Mvomero.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani
Jafo akilakiwa na wakazi wa Maguruwe wilayani Mvomero.
Wananchi wakicheza ngoma za kiluguru walipompokea Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo katika kijiji chao.
...........................................................................
Wakazi wa kijiji cha
Maguruwe wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wameishukuru serikali ya awamu
ya tano kwa kuwathamini na kuweza kufika kwenye kijiji hicho mteule wa Rais
ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo, kwa kuwa
hakuna kiongozi wa ngazi ya Uwaziri ambaye amewahi kufika kwenye eneo hilo.
Kutokana na Waziri
Jafo kuwa Waziri wa kwanza kufika kwenye kijiji hicho wazee wa kimila wa kijiji
hicho walimsimika na kumpa heshima maalum ya waluguru.
Wakizungumza huku
wakiwa wamejawa na furaha, Wananchi hao wamesema kijiji chao ambacho kipo juu
kabisa ya safu za milima ya Ulugulu hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya
uwaziri aliyewahi kufika maeneo hayo kwa kuwa barabara zake hazipitiki
kirahisi.
Wamesema
wamefurahishwa na kiongozi huyo kwa kuweza kuwafikia walipo hali ambayo
imewafanya kujisikia furaha.
Katika ziara hiyo ya
kikazi, Waziri Jafo amefanikiwa kuzindua vyumba vitatu vya madarasa vilivyojengwa
na Taasisi ya CDTF.
Hata hivyo, kutokana
na changamoto kubwa ya barabara katika eneo hilo, Waziri Jafo alimuagiza meneja
wa TARURA wilaya ya Mvomero kufanya tathmini ya barabara hiyo ili serikali ione
jinsi ya kuifanyia kazi hapo baadae ili wananchi hao waweze kuondokana na adha
hiyo.
0 comments:
Post a Comment