Mkurugenzi Mkazi wa shirika la AMREF
Dr.Florence Temu akitoa salamu zake kwa Makamu wa Rais, kabla ya
kukutana kwenye kikao cha ndani kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Simiyu.
Miongoni mwa wadau hao ni pamoja na shirika la AMREF Health Africa ambapo makamu wa Rais Mhe.Suluhu amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo Dr.Florence Temu. Ziara ya Makamu wa Rais iliyoanza jumapili Februari 18,2018 mkoani Simiyu inatarajia kufikia tamati kesho alhamisi.
Shirika la AMREF linatekeleza mradi wa Uzazi Uzima unaofadhiliwa na shirika la Global Affairs Canada (GAC) pamoja na washirika wengine ambao ni Marie Stopes Tanzania na Deloitte ambapo mradi huo unatekelezwa katika halmashauri za Bariadi Vijijini, Bariadi Mjini, Busega, Itilima, Meatu pamoja na Maswa ukilenga kuboresha huduma za afya ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Mkurugenzi
Mkazi wa shirika la AMREF Dr.Florence Temu akitoa salamu zake kwa
Makamu wa Rais, kabla ya kukutana kwenye kikao cha ndani kilichofanyika
Bariadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu. Na BMG
0 comments:
Post a Comment