Na Mwandishi Maalum- Mara
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amewaagiza maafisa ardhi na
watendaji wa serikali kuhakikisha wanawafuata wananchi wenye matatizo ya ardhi
katika maeneo yao ili kutatua migogoro ya ardhi.
Katika kutekeza suala
hilo kwa ufanisi, Mabula amewataka
watendaji kutoa matangazo wakati wa kuenda kutatua migogoro ya ardhi kwa
kuwaeleza wanachi ni lini wanaenda
katika maeneo yao kuwasikiliza na kwatolea majibu huko waliko.
‘’muende kila kijiji
kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao na mnapoenda huko muwatangazie kama
siku fulani mtaenda kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi’’ alisema mabula
Akiwa katika ziara yake
katika wilaya ya Butiama mkoani Mara Mabula amewataka watendaji kukaa siku
mbili tu ofisini na siku tatu katika wiki wawe maeneo ya tukio kwani serikali
inahitaji kumaliza migogoro ya ardhi kwa kuwafuata wananchi huko waliko.
Katika hatua nyingine,
naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula ameagiza
maeneo ya taasisi za serikali kupimwa na kupatiwa hati miliki. Ameshangazwa na
baadhi ya halmashauri kushindwa kupima hata taasisi moja ya serikali.
Amesema, katika
mazingira kama hayo ya taasisi za serikali kutopimiwa maeneo yao, ni vigumu
kabisa kukosekana migogoro na kubainisha kuwa
serikali haitaki kuwabomolea wananchi
kwa kuingia maeneo yasiyo miliki yao na kushauri maeneo ya serikali
kuwekewa alama.
‘’kunakuwa na migogoro
mingi ya wananchi na umma kwa sababu maeneo mengi hayajapimwa hivyo nashauri halmashauri zitenge fedha kwa
ajili ya kupima maeneo ya umma na
zinaweza kuanza kupima hata kwa shule na
ofiisi za watendaji kadhaa ‘’ alisema Mabula
Pia naibu waziri wa
ardhi nyumba na maendeleo ya makazi amesisitiza matumizi ya mfumo mpya wa
ulipaji kodi ya ardhi uzingatiwe na kila kitu kifanyike kulingana nilizowekwa.
Aidha, ameagiza
watendaji kuhakikisha wanasimamia
zoezi zima la utatuaji migogoro ya ardhi
katika maeneo husika kwa kugharamia pesa ya nauli badala ya suala hilo
kuachwa kwa walio katika mgogoro kugharamia
kwani linaweza kuwa kichocheo cha rushwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi
0 comments:
Post a Comment