Na Mwamdishi Maalum – Musoma
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Angelina Mabula amesema ni marufuku halmashauri
kuchukua maeneo ya wananchi bila ya kuwalipa fidia.
Mhe. Mabula amesema
hayo Wilayani Butiama mkoa Mara wakati
wa ziara yake yenye nia ya kutatua migogoro ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa
ukusanyaji kodi ya ardhi.
Amesema wakati wa
mchakato wa kuchukua maeneo ya mwananchi ni vyema wahusika wakashirikishwa kuanzia
hatua ya awali sambambana na kuelimishwa
juu ya zoezi hilo ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea.
‘’cha msingi ni kuanza
kuzungumza na mwananchi kabla ya kuchukua eneo lake na kumueleza eneo ambalo
ataachiwa na halmashauri zihakikishe mwananchi huyo anapimiwa pamoja na
kupatiwa hati yake’’ alisema Mabula
Aidha, mhe. Mabula
amesema eneo litakalochukuliwa na halmashauri viwanja vyake kuuzwa fedha
itakayopatikana halmashauri ihakikishe
inatumika katika kutengeneza miundo mbinu na huduma nyingine za jamii na
kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo
migogoro haiwezi kutokea.
Naibu waziri wa ardhi
nyumba na maendeleo ya makazi ameziagiza halmashauri kuhakikisha zinapanga miji
kulingana na ‘master plan’ ili kuwa miji bora iliyopangika
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi
22 Februari, 2018
0 comments:
Post a Comment