Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la
uchimbaji madini ya makaa ya mawe katika kijiji na Kata ya Magamba baada ya
kuwasili kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya uchimbaji madini Mkoani Songwe, Leo
23 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na
kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Mbozi mara baada ya kuwasili kwa ziara ya
kikazi kukagua miradi ya uchimbaji madini Mkoani Songwe, Leo 23 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la
uchimbaji madini ya makaa ya mawe katika kijiji na Kata ya Magamba baada ya
kuwasili kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya uchimbaji madini Mkoani Songwe, Leo
23 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Songwe
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameagiza wamiliki
wa kampuni za uchimbaji wa Madini kote nchini kuwapatia mikataba ya kazi
wafanyakazi wote pasina kubagua.
Mhe Biteko ametoa agizo hilo Leo 23 Februari 2018 wakati
alipotembelea eneo la uchimbaji wa makaa ya mawe katika Kijiji na Kata ya
Magamba, Wilayani Mbozi linalomilikiwa na kampuni ya Magamba Coal Mine.
Alisema amejiridhisha kuwa wafanyakazi wengi katika migodi
mbalimbali nchini ukiwemo wa Magamba hawana mikataba jambo ambalo linafifihisha
uhakika wa ajira zao.
Aidha, Naibu Waziri huyo wa Madini ametoa siku 14 kuanzia Leo 23
Februari 2018 mpaka 9 Machi 2018 kwa kampuni ya Magamba Coal Mine kuwa
wamekamilisha taarifa ya utekelezaji wa maelekekezo ya ukaguzi wa migodi
yaliyotolewa kwao na Ofisi ya Madini kanda hiyo.
Alisema kuwa endapo watashindwa kufanya hivyo ni wazi kuwa
watakuwa wamekiuka masharti ya leseni zao na wajibu wao kwa jamii
inayowazunguka na hivyo Wizara itawachukulia hatua bila kuchelewa.
Sambamba na hayo pia kampuni hiyo imetakiwa kuboresha na kuwa na
mahusiano chanya na kijiji cha Magamba na serikali kwa ujumla ikiwemo kusaidia
kuboresha baadhi ya maeneo ikiwemo sekta ya afya na elimu.
Naibu Waziri wa Madini akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa
wa Songwe alisema kuwa serikali imekusudia kurejesha uchumi fungamanishi kwa
wananchi hivyo kampuni haziwezi kuwa na uchumi imara kama zitasalia kuendesha
migodi pasina utaratibu wa kisheria.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment