METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 23, 2018

KAMPENI YA KUFICHUA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI KUANZA WILAYANI NACHINGWEA

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango anatarijia kuanzisha Kampeni ya kufichua watoto wenye vichwa vikubwa (Hydrocephalus) na mgongo wazi (Spinal Bifida) katika Wilaya hiyo.

Katika kampeni hiyo Ofiai ya Mkuu wa Wilaya hiyo itashirikiana na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) ili kurahisisha huduma hiyo kwa wananchi wenye uhitaji wa huduma hiyo.

Katika kukamilisha kampeni hiyo Mhe Muwango anawalika wananchi wote wa Wilaya ya Nachingwea na wilaya za jirani kuwafichua watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ili wapate tiba na ushauri wa kitaalamu BURE.

Kampeni hiyo itaongozwa na Kauli mbiu isimayo "Usimfiche mtoto, kichwa kikubwa na mgongo wazi vinatibika".

Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com na www.wazohuru.com Mhe Muwango alisema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kufika Zahanati ya karibu, Kituo cha afya, Hospitali ya Wilaya au Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nachingwea.

MWISHO

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com