METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 2, 2018

Kamati ya Taifa yapitisha mbegu mpya

Kamati ya Taifa ya kupitisha mbegu mpya (NVRC) imepitisha  matumizi aina 25 ya mbegu mpya za mazao mbalimbali ya kilimo ambapo aina nane zimetafitiwa na Taasis binafsi na aina 17 zimetafitiwa na Taasisi za serikali.

Kamati ilikutana kwa muda wa siku tatu mfululizo katika ukimbi wa mikutano wa Tasisi ya utafiti wa Miwa Kibaha  ambapo mbegu hizo zilipitishwa.

Aidha Kikao hicho ambacho Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Eng. Methiw Mtigumwe alikuwa mwenyekiti amewataka watafiti na wazalishaji kuongeza uzalishaji wa mbegu hizo na kuzitangaza ili ziweze kuwafikia wakulima.

Mazao hayo ni aina 3 za mahindi, tisa za maharage,moja ya mpunga,tatu karanga, njugu mawe mbili pamba aina mbili na aina tano za tumbaku.

Hatua hiyo ya kamati inalenga kuongeza uzalishaji na tija pamoja na kuinua kipato kwa mkulima.

Kupitishwa kwa aina hizo mpya za mbegu kunatokana na mapendekezo yalifanywa na kamati ya taifa ya kitaalamu ya kuhakiki aina mpya za mbegu za mazao ya kilimo.

Aidha mbegu hizo zimepitishwa baada ya kufanyiwa utafiti wa kina, na kubainika kuwa zina sifa mbalimbambali kama vile kutoa mavumomengi ukinzai dhidi ya magonjwa, kukomaa mapema na kupendwa na wakulima.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com