METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 2, 2018

DKT MWIGULU AZINDUA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA WANANCHI KWA AJILI YA KITAMBULISHO CHA URAIA MKOANI TABORA

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba akizindua zoezi la uandikishaji wa wananchi kupata kitambulisho cha uraia mkoani Tabora kushoto kwake ni kaimu mkurugenzi mkuu wa NIDA Andrew Masawe na mkuu wa wilaya ya Tabora Queen Mlonzi. zoezi hilo lilifanyika leo 2 Februari 2018 katika wilaya ya Tabora

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba akingalia jinsi idara ya uhamiaji inavyoshiriki kuhakiki raia sahihi wa Tanzania katika uandikishaji wananchi kupata kitambulisho cha utaifa mkoa wa Tabora.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba amewataka watanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa kwani si zoezi la hiari ni lazima kwa mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi ili kutambukiwa.

Waziri Mwigulu amewataka wananchi waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania .

"Zoezi hili ni bure kujiandikisha na kupata kitambulisho pasitokee kiongozi yeyote wa wilaya na vijiji kuchangisha fedha wananchi ili wapate fomuza kujiandikisha na wala zoezi hili lisiunganishwe na siasa."alisema Dr.Mwigulu
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com