METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, January 11, 2018

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGIA SHUGHULI ZA MAENDELEO






Wananchi wa Jimbo la Ilemela wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika uchangiaji wa shughuli za maendeleo

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu wa kata za Shibula, Kahama na Buswelu kupitia ziara yake ya Jimbo kwa kata zote za wilaya hiyo kueleza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi aliyokabidhiwa mara baada ya kushinda ubunge ambapo amewaasa kuhakikisha wanachangia shughuli za kimaendeleo ikiwemo uchangiaji wa huduma za afya, miundombinu, maji, umeme na elimu huku akikumbusha wajibu wa wazazi, kamati za shule na jamii katika suala zima la kufanikisha elimu bila malipo

‘… Ndugu zangu elimu bila malipo haiondoi wajibu wako kama mzazi, haiondoi wajibu wako kama jamii hivyo ni lazima tuchangie shughuli za maendeleo ili kusaidia watoto wetu tusiachie Serikali kila kitu, Kila mmoja anawajibu wake, Kamati za shule zinawajibu wake na bodi za shule zina wajibu wake …’ Alisisitiza

Aidha Dkt Angeline Mabula amekemea tatizo la mimba za utotoni , amefafanua juu ya umuhimu wa zoezi la urasimishaji makazi na umilikishwaji wake pamoja na kumshukuru Mhe Rais Dkt John Magufuli kwa sera ya Elimu Bure na msaada wa gari la kubebea wagonjwa alilolitoa kwa hospitali ya Sangabuye Ilemela huku akiwataka wananchi kumuunga mkono kwa kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali kupitia Ilani hiyo ya Uchaguzi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Buswelu Mhe Sarah Ng’wani amewataka wajumbe wa halmashauri kuu wa kata yake kuwa chachu katika kuhamasisha shughuli za kimaendeleo na kuwa wavumilivu ili kuwapa nafasi wawakilishi waliowachagua kutekeleza yale yaliyoelezwa katika Ilani ya Uchaguzi.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Shibula Ndugu Amos Lungisa amewataka wananchi wa kata yake kutokatishwa tama wanapojitoa kufanikisha shughuli za maendeleo sanjari kuwaunga mkono viongozi wao waliowachagua.

Katika Ziara hiyo ya utekelezaji wa ilani aliambatana na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi na jumuiya zake zote kwa ngazi ya wilaya na watendaji wa Serikali kwa kata zote zilizohusika wakiongozwa na katibu wa Itikadi na Uenezi wa wilaya hiyo

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Ilemela 
11.01.2018
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com