METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, January 11, 2018

DC MUWANGO AKABIDHI MIL 86 KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI WILAYANI NACHINGWEA

Na Mathias Canal, Wazo Huru Blog

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango jana Tarehe 11 Januari 2018 amekabidhi kiasi cha shilingi milioni 86,000,000 kwa vikundi vya kina mama, vijana na walemavu kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi katika jamii.

Mhe Muwango amekabidhi fedha hizo zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ambazo ni asilimia 10% ya mapato yake ya ndani kwa kipindi cha nusu mwaka yaani Julai 2017 - Desemba 2017.

Alisema kuwa kutolewa kwa fedha hizo ni Utekelezaji wa sera ya uwekezaji wa kiuchumi kwa wananchi ambapo hata hivyo kwa usimamizi mzuri kwa Halmashauri imelazimika kutekeleza kwa asilimia 100%

Akizungumza wakati akiwakabidhi wajasiriamali hao Mhe Muwango aliwakumbusha wajasiliamali haki na wajibu wao kwa kuwa na Nidhamu ya kufanya jambo lililokusudiwa kwa manufaa yao bila kubadili matumizi ya fedha hizo.

Aliongeza kuwa wananchi hao wanatakiwa Kufanya kazi kwa bidii, weledi na ubunifu ili waweze Kurejesha fedha za mkopo kwa wakati na kutunza kumbukumbu kwa ufasaha.

Mhe Muwango alielekeza kuwa wataalamu mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea wanapaswa kupatiwa elimu juu ya ujasiliamali lakini pia kuwatembelea mara kwa mara na kujua changamoto wanazo kabiliana nazo ili kutoa ushauri utakaowasaidia kuimarika kiuchumi.

Alisema kuwa endapo wakifanya vizuri itakuwa hatua nzuri ya kuongeza kiwango cha mikopo ambapo hata hivyo amewahisi wataalamu hao kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya wajasiliamali na kubiresha huduma muhimu.

Dc Nachingwea Mhe Muwango Alisisitiza kuwa Serikali imeshaandaa mazingira ya kumsaidia mjasiliamali Kwa kuimarisha miundombinu ili kuyafikia masoko ndani na nje ya Wilaya ya Nachingwea.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com