METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, January 14, 2018

MGODI WAFUNGWA KWA MUDA KUFANYA KAZI

Na; Asha Shaban, Butiama

Naibu waziri wa madini  Stanislaus Nyongo jana ameufunga kwa mda mgodi wa Zem T co.Ltd wa wilayani bunda mkoani Mara kwa kusindwa kukidhi mashariti.

Naibu waziri nyongo alisema kuwa mnamo mwezi Desemba aliweza kufika mgodini hapo na kukuta hali  za wafanyakazi kutokuwa na ubora.

Alisema kuwa aliwaandikia barua mgodi huo kuwataka kukidhi vigezo vya kuwapa  wafanyakazi vitendea kazi pamoja mikataba na kuwapatia mishahara kima cha chini kwa wafanyakazi wanao stahili.

"Nimekuja kikagua Leo lakini bado hamjatekeleza maagizo yangu kwanza mmewapa vifaa kwa kuwalipisha kinyume na utaratibu"alisema

" Naagiza kuanzia kesho mgodi kusimamisha shughuli zote za utendaji mpaka pale mtakapo kamilisha utaratibu nilio wapatia "

"Timu yangu ya ukaguzi itakuja kukagua kama mmefanya marekebiaho ambayo nimeagiza na muyatekeleze ndipo muanze kazi"

"Naagiza mkimaliza mtaniita kuja kuangalia ndipo muanze kazi tena ikiwa ni pamoja na kuwarudisha kazini wafanyakazi ambao mliwafukuza kazi"

Kwa upande moja wa wafanyakazi moses kagari amesema  mshaara wake ulikata kiasi cha shilingi elfu 30 kwa ajili ya kulipia gambuti na kofia ngumu za kufanyia kazi.

Naye Afisa mahusiano wa mgodi huo Samuel nyoingo alisema wamepokea mamuzi hayo ya waziri kwa kufunga mgodi huo kwa mda na watafanyia marekebisho walioambiwa.

Alisema japo itakuwa inawaadhiri watu wengi lakini hawana budi kurekebisha makosa hayo na itawachukua kama muda wa wiki moja kukamilisha maagizo yote ya Naibu Waziri wa Madini na kuanza kufanya kazi tena.

Mwisho
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com