Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi zawadi ya mwanafunzi bora kitaaluma ngazi ya Stashahada ya Uhasibu na Uongozi Ndg Methusela Piniel kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi zawadi ya mwanafunzi bora kitaaluma ngazi ya Shahada ya Biashara na Uchumi Bi Diana Kibodya kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Prof Faustine K. Bee akitoa taarifa ya chuo hicho kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi sambamba na baadhi ya wahitimu kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma chuoni hapo tarehe 6 Disemba 2018.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro
Imebainika
kuwa tafiti na machapisho mengi yanayofanywa na wanataaluma na wanafunzi katika
Vyuo mbalimbali si tu zinasaidia kujenga taswira za vyuo bali zinapaswa kuwa
sehemu ya kufanya elimu iwe nzuri na bora zaidi.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 6 Disemba 2018
wakati akizungumza kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi
waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Mhe
Hasunga amewaagiza watendaji wa Chuo hicho sambamba na vyuo vingine nchini
kufanya tafiti za kutosha katika tasnia ya ushirika na kuhakikisha kuwa Matokeo
ya tafiti hizo yanawafikia walengwa. "Serikali nayo kwa upande wake
imeweka na itaendelea kuweka mazingira rafiki zaidi yatakayosaidia kuimarisha
dhana ya ushirika miongoni mwa jamii ya watanzania" Alisema
Alisisitiza
kuwa moja ya kadhia inayovikumba vyuo mbalimbali nchini ni kutowekwa wazi kwa
haraka machapisho na Tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutangaza ili
zijulikane katika sehemu mbalimbali Duniani.
"Ndugu
zangu hakuna nchi inaweza kuendelea bila kuwekeza kwenye utafiti hivyo ni
lazima kuongeza jitihada na juhudi katika utafiti" Alisisitiza
Alisema
kuwa Vyuo vikuu vinatambuliwa kama taasisi zilizobobea katika kufundisha,
kujifunzia, kufanya tafiti na kutoa huduma za ushauri hivyo vinapaswa kutangaza
matokeo ya Tafiti wanazozifanya.
Alisema,
kupitia elimu hiyo itolewayo na vyuo vikuu, maarifa, ujuzi na mtazamo chanya
kwa maendeleo vinaweza kujengwa, kuboreshwa, kuendelezwa na kusambazwa kwa
walengwa mbalimbali. Kwa msingi huo, utoaji elimu bora inayokidhi viwango na
inayoendana na mahitaji ya soko lazima izingatiwe.
Akizungumzia
Ushirika, Mhe Hasunga amesema kuwa Ushirika ni dhana ya kujisaidia wenyewe
katika maendeleo. "Hatuna budi sisi kama wadau wa ushirika kuhakikisha
kuwa tunajenga misingi imara ya elimu ya ushirika kwa wadau wetu ili waweze
kujikwamua katika wimbi la umaskini kwa kuanzisha shughuli zenye tija (kwa
mfano ushirika wa viwanda) zitakazowapatia kipato cha uhakika" Alisisisitiza
Aidha,
Waziri Hasunga ameupongeza uongozi Wa chuo kikuu cha Ushirika Mosho kwa
kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya Ushirika nchini kwa
kuandaa na kutoa wataalamu katika sekta ya Ushirika kuanzia ngazi ya
Astashahada, Stashahada hadi shahada za awali, Umahiri na Uzamivu.
Akitoa
maelezo ya awali Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Prof Faustine K.
Bee wakati akimkaribisha mgeni rasmi alisema kuwa sekta ya Kilimo imekumbwa na
changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na Ushirika kama dhana kuwa na mtazamo
hasi kwa baadhi ya watu inayosababishwa na uendeshwaji Wa Ushirika usiokuwa na
tija kwa wanachana, jamii na Taifa kwa ujumla.
"Vilevile
migogoro ya Mara kwa mara katika vyama vya Ushirika kutokana na kuwepo kwa watu
wachache wasiowaaminifu na kukosa maadili" Alikaririwa Prof Bee
Alisema
Chuo hicho kinatambua kuwa vyama vya Ushirika ni vyombo muhimu sana katika
utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa
miaka mitano (2016/2017) - (2020/20121), Malengo yavMaendeleo endelevu 2030
pamoja na ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment