Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewahakikishia wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Manispaa hiyo kupata nafasi pasina wasiwasi.
Kayombo ameyasema hayo Jana tarehe 8/01/2018 wakati akiwa ziarani Katika shule mpya kabisa ya Sekondari Kimara Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika ziara hiyo MD Kayombo aliambatana na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Bi Neema Maghembe pamoja na timu ya wataalamu wengine kutoka katika idara ya Elimu Sekondari Manispaa ya Ubungo.
Mkurugenzi Kayombo katika ziara hiyo aliweza kukagua Jengo jipya kabisa la shule ya Sekondari lenye vyumba vinne vya Madarasa pamoja na samani zilizoko katika madarasa hayo kama madawati na meza.
Pia Kayombo alisikiliza kwa makini changamoto kutoka kwa mwalimu Mkuu wa shule hiyo ambayo tayari imeshapokea wanfunzi wa kwanza kuanza kidato cha kwanza mwaka 2018
Baada ya kusikiliza kwa makini changamoto hizo Mkurugenzi Kayombo alisema "napenda nikuhakikishie mwalimu wangu na walimu wengine wote katika Manispaa ya Ubungo suala elimu kwangu si la mchezo mchezo nitajipanga kupunguza changamoto kama sio kuzimaliza kwa kadri iwezekanavyo" .
Aidha ifahamike kuwa Kata ya Kimara kwa muda mrefu haikuwa na shule ya Sekondari licha ya Kata hiyo kuwepo toka enzi za Manispaa ya Kinondoni kwa sasa tumejenga shule hiyo ya Sekondari Kimara kwa kutumia fedha za ndani (own source)
Kwa kuwa Manispaa ya Ubungo imejipanga kuondoa kama sio kumaliza kabisa vikwazo vinavyoathiri mazingira bora ya ujifunzaji na ufundishaji ikaamua kutumia fedha za mapato ya ndani ya Manispaa kujenga madarasa hayo na sasa yanatumika.
Kwa pamoja Ubungo tunasonga mbele
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
0 comments:
Post a Comment