METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, January 18, 2018

JAFO AAGIZA UKARABATI WA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA UKAMILIKE HARAKA



Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ameagiza ukarabati wa miundombinu ya sekondari ya Kibaha ukamilike haraka ili wanafunzi waweze kupata mazingira mazuri ya kusomea. 

Shule ya sekondari Kibaha ni miongoni mwa shule zilizo katika mpango kabambe wa ukarabati ambapo takribani shule kongwe 89 zinafanyiwa ukarabati ili ziweze kuwa katika mazingira rafiki ya utoaji wa elimu bora hapa nchini.

Kutokana na ukarabati huo, leo Waziri Jafo amtembelea shuleni hapo na kukagua ukarabati wa shule hiyo.


Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ametaka ukarabati huo ukamilike kwa muda uliopangwa ili wanafunzi waweze kusoma kwenye mazingira mazuri.

Aidha, Jafo ameendelea kutoa msisitizo kwa walimu wote kutotoza gharama za aina yeyote kwa wanafunzi kama alivyo elekeza Mhe. Rais John Magufuli kwani kumzuia mwanafuzi kupata elimu ni kosa kubwa lisilovumilika.

Kwa upande wao, Wanafunzi wa kidato cha sita wa Kibaha Sekondari wameahidi kwamba katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu watapambana ili washike nafasi tatu bora kitaifa. 

Kadhalika, Wakala wa Majengo nchini (TBA) wameahidi kwamba ifikapo Januari 25 mwaka huu watakuwa wamekamilisha ujenzi wa bweni la  kibo ili waweze kuhamia kukarabati mabweni mengine pamoja na madarasa. 
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com