Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati akifunga kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akimnadi mgombea Udiwani Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo kwenye mkutano wa hadhara wakati akifunga kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Ndg Kheri Denice James akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati akifunga kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018.
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara za ufungaji wa kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018.
Na Mathias Canal, Arusha
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa
nchini Tanzania hakuna Chama chenye uwezo wa kushindana na CCM kwani vyama vilivyopo
ni mfano wa kamati za harusi zenye jukumu la kupanga na kuratibu sherehe za
ndoa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo na Mjumbe wa
Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James wakati akifunga kampeni za
uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha unaotarajiwa
kufanyika kesho 13 Januari 2018.
Kheri amebainisha kuwa pamoja na wananchi kufanya maamuzi ya ama
kuchagua jiwe au mtu mwaka 2015 Arusha walipata hasara kubwa kwani matatizo yao
yalikosa mtu wa kuyasemea bungeni katika kipindi cha takribani miaka saba sasa.
Alisema kuwa wananchi Mkoani Arusha walifanya makosa Octoba 25,
2015 katika uchaguzi Mkuu kwa kuchagua wawakilisha wa Ubunge na Udiwani
wasiokuwa na mtazamo wa kuwasaidia badala yake kujinufaisha wao pekee pasina
kujali umuhimu na maslahi makubwa ya wananchi na watanzania waliowachagua.
Alisema kuwa katika kipindi kirefu serikali ya Chama Cha
Mapinduzi imekuwa ikizalilishwa na kutukanwa na watanzania waoishi ndani na nje
ya nchi lakini imekuwa na uvumilivu mkubwa kwa ajili ya maslahi ya watukanaji
na wananchi wote kwa ujumla wake.
Aliongeza kuwa Tanzania katika kipindi hiki imepata Rais
anayewapenda na kuwajali wananchi wanyonge ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM
Taifa Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliyeleta heshima kubwa kwa kila mwananchi
kutokana na maamuzi yake ya kutaka watanzania wote wanufaike na kufaidi matunda
ya rasilimali zao.
Aidha, Alisema kuwa katika kipindi kifupu tangu kuteuliwa kwa
Mhe Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ubabaishaji umekwisha Mkoani humo
kwani wananchi wametambua uduni wa busara kwa viongozi waliowachagua
wanaotokana na vyama vya upinzani.
Alisema Mhe Gambo amekuwa ni kijana mzalendo na alama bora
katika Taifa hivyo mwananchi wanapaswa kumuunga mkono katika utendaji wake
kwani kazi ya uongozi ni kazi kubwa na ngumu sana endapo kama kuna watu watakukwamisha
kwa makusudi.
Sambamba na hayo pia Mwenyekiti Kheri alimnadi Mgombea Udiwani
kwa tiketi ya CCM katika Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo na kumtaka mara
baada ya kuchaguliwa anapaswa kuhakikisha anaboresha huduma za afya, elimu, na
miundombinu haraka iwezekanavyo katika Kata hivyo kwa mujibu wa maelekezo ya
ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment