METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 5, 2017

Siku ya Ukimwi Duniani 2017, Timu za Sanvik na Mantrac zachuana vikali Mwanza

Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Sandvik Fc imetoa kichapo cha goli 4-3 dhidi ya wapinzani wao Mantrac Tanzania  za jijini Mwanza katika mchezo wa  kirafiki uliotimua vumbi katika uwanja wa Nyamagana.
Mchezo huo ulioandaliwa na kampuni ya Sandvik Mining and Construction (T) LTD ambao waliwakaribisha wenzao wa Mantrac Tanzania, kwa ajili ya kuungana na watanzania na dunia kwa ujumla katika kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani inayofanyika kila mwaka Disemba Mosi.
Sandvik FC ilifunga magoli kupitia washambuliaji wake Petro Ng’ oko dakika ya 13, Samwel  Manga dakika ya 48 na Hamis Luhenga dakika ya 60 na 72, huku Mantrac ifunga kupitia Emmanuel Joel dakika ya 10, na Hamfrey Kirutu dakika 30 na 52.
Akizungumza na BMG, Afisa Rasirimali Watu (HR) wa Sandvik Mining and Construction (T),  Deogratias Sendama  ambaye ni Nahodha Msaidizi wa timu hiyo,alisema, mchezo huo ni kwa ajili ya kuungana na watanzani na dunia katika kuadhimisha siku ya ukimwi dunia, pia ulikua mzuri na amefurahi kuwafunga wapinzani wao na hatimaye kuibuka na ushindi.
Sendama alisema wataendelea kufanya mazoezi ili kuimarisha kikosi zaidi, kwani mchezo ni afya na husaidia kuimarisha mahusiano kama walivyofanya wao.
Pia aliwaomba, wafanyakazi wajitokeze kushiriki  katika michezo na mazoezi,ili kuimarisha afya na kuepusha mwili kuwa dhaifu pamoja na kuondokana na msongo wa mawazo.
Kwa upande wake nahodha wa  timu ya Mantrac Tanzania  Emmanuel Joel alisema, mchezo ulikua mzuri na walicheza vizuri japo kuna makosa ya kibinadamu,hivyo wanajipanga kwa kufanya mazoezi ili katika mechi nyingine waweze kufanya vizuri kwani hii walishtukizwa.
Wafanyakazi wa kampuni ya Sandvik Mining and Construction (T) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki katika uwanja wa Nyamagana na kuibuka na ushindi wa goli 4-3 dhidi ya Mantrac Tanzania kwenye Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, Disemba Mosi,2017.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com