Judith Ferdinand, Mwanza
Ligi daraja la tatu mkoa wa Mwanza msimu wa 2017/2018 imepangwa kuanza kutimua vumbi Disemba 29 mwaka huu ambapo 48 zinatarajiwa kushiriki.
Katika ligi hiyo ada ya ushiriki ni shilingi laki mbili kwa kila timu na zoezi la utoaji fomu litaanza Disemba sita na kufungwa Disemba 20 mwaka huu.
Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA), Leonard Malongo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi ofisini kwake jijini Jijini Mwanza.
Malongo alisema ikao cha Kamati Tendaji cha MZFA kilichokaa Disemba Mosi kiliamua ligi daraja la tatu ianze tarehe 29 mwezi huu ambapo kilipendekeza kuwepo kwa vituo vitano ambavyo ni Kwimba, Magu, Nyamagana, Ukerewe na Sengerema.
“Jumla ya timu 48 zitashiriki msimu huu wa ligi daraja la tatu, ambazo ni timu 29 zilibaki msimu uliopita, 14 kwa mujibu wa kanuni ambapo kila wilaya inatakiwa kutoa timu mbili mshindi wa kwanza na wapili wa ligi daraja la nne, pia kufuatia maombi ya baadhi ya FA wilaya ya kuomba kuongezewa timu na kamati tendaji ya MZFA ilikubali kwa wilaya iliyochezesha timu 20 na kuendelea ligi wilaya kuongezewa timu moja ambayo wataleta mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu,hivyo wilaya zilizopata bahati hiyo ni Nyamagana, Ilemela, Magu,,Misungwi na Ukerewe,” alisema Malongo.
Alisema wadau wanatakiwa kusapoti timu ili zijiandae ipasavyo na kuwezesha mkoa kupata timu bora itakayoshiriki ligi daraja la pili ngazi ya taifa kwani kwa sasa mkoa hauna timu inayoshiriki ligi hiyo.
Hata hivyo alisema, wanazungumza na makampuni mbalimbali ambao yataweza kudhamini ligi hiyo,ili kuondoa changamoto pamoja na kuleta hamasa kwa wachezaji.
Aidha alisema wakimaliza kuzungumza na wadhamini ndio watajua zawadi gani watatoa kwa mshindi wa kwanza mpaka watatu.
Kadhalika alisema katika kuhakikisha wanalinda mapato katika ligi hiyo watatengeneza vitambulisho kwa wadau maalumu kama wanahabari na wengine watalipia kiingilio ili kushuhudia mechi zitakazokuwa zinachezwa,sambamba na kuwalipa waamuzi madeni yao kabla ya ligi hiyo kuanza na kufanya kuwa bora.
0 comments:
Post a Comment