METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 8, 2017

SERIKALI WILAYANI GEITA KUWACHUKULIA HATUA KALI WATAKAO HUJUMU ZOEZI LA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,akizindua zoezi la usajili wananchi kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa ,  kwenye halmashauri ya Mji wa Geita ,Mratibu wa NIDA Mkoani Geita,Emmanuel Ernest akitoa maelekezo ya namna ya kutumia kifaa cha usajili.
Mratibu wa NIDA Mkoani Geita,Emmanuel  Ernest akizungumzia madhumuni ya uandikishaji wananchi kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa kwenye halmashauri ya mji wa Geita.
Watoto wa kituo cha Brith light wakiimba wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya wadau wakiwatunza.


Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi kulia ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Constatine Molandi akifuatiwa na diwani wa kata ya kalangalala,Sospeter Mahushi wakiwa kwenye zoezi la uzinduzi wa vitambulisho.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinaly akizungumza na wananchi juu ya umuhimu wa zoezi la uandikishwaji vitambulisho vya Taifa.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akisisitiza viongozi wa mitaa ambao wataonekana kuhujumu zoezi la usajili wananchi kwenye vitambulisho vya Taifa watachukuliwa hatua kali.


Wananchi ambao wamejitokeza kujiandikisha wakiwa kwenye mstaari wakisubilia shughuli za kujisajili kwaajili ya kupata vitambulisho vya Taifa.

Na,Joel Maduka,Geita

Serikali Wilayani Geita imesema haitamuhurumia yeyote atakayehujumu zoezi  la uandikishaji kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo wa zoezi la kuwasajili wananchi kwenye halmashauri ya mji wa Geita, Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi alisema kituo chochote ambacho zoezi hilo halitaenda vizuri, hatua zitachukuliwa dhidi ya Mwenyekiti na mtendaji wa mtaa husika.

“Hatutakuwa na huruma na mtu yoyote ambaye hatahusika na kuhujumu zoezi hilo na kama tukisikia mwenyekiti wa mtaa na mtendaji kunatatizo ambalo limetokea tutakushughulikia hapo hapo na kama ni mwenyekiti wa mtaa sio kukushughulikia tu nitafuta nafasi yako tutachagua kiongozi mweningine hatutaki watu wasio na maadili kwenye Wilaya yetu.”Alisisitiza Kapufi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Mhandisi Modest Apolinary amewasisitiza wananchi kutumia nafasi hiyo kwa kuwa haitajirudia tena.
“Ni waombe tu wananchi kwamba hii nafasi ambayo mmepewa  ni nafasi ya kipekee sana haitajirudia tena kwa hiyo ni zamu ya wananchi wote kuhakikisha kwamba mnajitokeza kwa wingi kujiandikisha ili muweze kupata vitambulisho vyenu”Alisema Modest.

Mratibu wa NIDA Mkoani Geita Bw Emmanuel Ernest amesema wameanza usajili tarehe 23 August mwaka huu na kwamba wamesajili awamu 6 zenye jumla ya kata 12 na wananchi waliojiandikisha ni Laki moja, elfu 36 na 643 sawa na asilimia 75.33 na kwamba matarajio ni kuandikisha watu Laki moja elfu 81 na 374 hivyo waliobaki ni watu elfu 44 na 731.

Akielezea faida na umuhimu wa kitambulisho cha Taifa Mratibu alisema kuwa kitasaidia serikali kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato(kodi)pamoja na kuongeza idadi ya wanaotakiwa kulipa kodi,pia vitasaidia kupunguzia serikali gharama za kusafirisha daftari la wapiga kura,na kuwa daftari lenye taarifa sahihi za watu na mahali walipo.

Bi,Rosemary Yusuf ambaye ni mwananchi wa msalala road alisema vitambulisho  vya Taifa vitawasaidia kwani watatambulika kuwa wao ni watanzania  harari.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com