Serikali
Wilayani Geita imesema haitamuhurumia yeyote atakayehujumu zoezi la uandikishaji kwa ajili ya vitambulisho vya
Taifa.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo wa zoezi la kuwasajili wananchi kwenye halmashauri ya mji
wa Geita, Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi alisema kituo chochote
ambacho zoezi hilo halitaenda vizuri, hatua zitachukuliwa dhidi ya Mwenyekiti
na mtendaji wa mtaa husika.
“Hatutakuwa
na huruma na mtu yoyote ambaye hatahusika na kuhujumu zoezi hilo na kama
tukisikia mwenyekiti wa mtaa na mtendaji kunatatizo ambalo limetokea
tutakushughulikia hapo hapo na kama ni mwenyekiti wa mtaa sio kukushughulikia
tu nitafuta nafasi yako tutachagua kiongozi mweningine hatutaki watu wasio na
maadili kwenye Wilaya yetu.”Alisisitiza Kapufi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya mji wa Geita, Mhandisi Modest Apolinary amewasisitiza
wananchi kutumia nafasi hiyo kwa kuwa haitajirudia tena.
“Ni waombe
tu wananchi kwamba hii nafasi ambayo mmepewa ni nafasi ya kipekee sana haitajirudia tena kwa
hiyo ni zamu ya wananchi wote kuhakikisha kwamba mnajitokeza kwa wingi
kujiandikisha ili muweze kupata vitambulisho vyenu”Alisema Modest.
Mratibu wa
NIDA Mkoani Geita Bw Emmanuel Ernest amesema wameanza usajili tarehe 23 August
mwaka huu na kwamba wamesajili awamu 6 zenye jumla ya kata 12 na wananchi
waliojiandikisha ni Laki moja, elfu 36 na 643 sawa na asilimia 75.33 na kwamba
matarajio ni kuandikisha watu Laki moja elfu 81 na 374 hivyo waliobaki ni watu
elfu 44 na 731.
Akielezea
faida na umuhimu wa kitambulisho cha Taifa Mratibu alisema kuwa kitasaidia
serikali kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato(kodi)pamoja na kuongeza idadi ya
wanaotakiwa kulipa kodi,pia vitasaidia kupunguzia serikali gharama za
kusafirisha daftari la wapiga kura,na kuwa daftari lenye taarifa sahihi za watu
na mahali walipo.
Bi,Rosemary
Yusuf ambaye ni mwananchi wa msalala road alisema vitambulisho vya Taifa vitawasaidia kwani watatambulika
kuwa wao ni watanzania harari.
No comments:
Post a Comment